Pata taarifa kuu

Urusi inasema meli yake ya mafuta imeshambuliwa na Ukraine

Maofisa nchini Urusi wanasema Meli yake ya mafuta iliyokuwa na wafanyakazi 11 imeshabuliwa na Ukraine katika Bahari Nyeusi.

Kwa mujibu wa maofisa hao, sehemu ya meli hiyo iliharibiwa katika shambulio hilo la usiku kucha japokuwa hakuna yeyote aliyejeruhiwa
Kwa mujibu wa maofisa hao, sehemu ya meli hiyo iliharibiwa katika shambulio hilo la usiku kucha japokuwa hakuna yeyote aliyejeruhiwa AP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa maofisa hao, sehemu ya meli hiyo iliharibiwa katika shambulio hilo la usiku kucha japokuwa hakuna yeyote aliyejeruhiwa.

Hili ni shambulio la hivi karibuni kutokea katika bahari Nyeusi tangu Moscow mwezi uliopita kutangaza kujiondoa kwenye mkataba wa usafirishaji wa nafaka kati yake na Ukraine.

Vyanzo vya taarifa hii, meli hiyo ilikuwa imebeba idadi kubwa ya mafuta.

Meli hiyo ya mafuta na kemikali iko chini ya vikwazo vya Marekani kwa kusambaza mafuta ya ndege kwa wanajeshi wa Urusi nchini Syria wanaomuunga mkono Rais Bashar al-Assad.

Shirika la habari la serikali ya Urusi RIA Novosti limesema hakuna majeruhi katika shambulio hilo, likinukuu Kituo cha kuratibu uokoaji baharini cha Novorossiysk.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.