Pata taarifa kuu

Urusi inasema imeharibu ndege 20 zisizo na rubani za Ukraine

Nairobi – Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema kuwa vikosi vyake vimeharibu ndege 20 zisizo na rubani za Ukraine kwenye rasi ya Crimea inayokaliwa na Urusi.

Un soldat ukrainien portant un drone près de la ville d'Avdiïvka, dans la région de Donetsk, à proximité de la zone de combat, le 17 février 2023.
Un soldat ukrainien portant un drone près de la ville d'Avdiïvka, dans la région de Donetsk, à proximité de la zone de combat, le 17 février 2023. AP - LIBKOS
Matangazo ya kibiashara

Hakukuwa na majeruhi wala uharibifu wowote kutokana na jaribio hilo la shambulio, wizara ya ulinzi imesema kupitia mtandao wa Telegram.

Ndege kumi na nne zisizo na rubani ziliharibiwa na mifumo ya ulinzi wa anga na sita ziliharibiwa kupitia mfumo wa  kielektroniki kwa mujibu wa wizara hiyo.

Sergei Kryuchkov, mshauri wa gavana wa Crimea aliyewekwa na Urusi, alisema hapo awali kuwa mifumo ya ulinzi wa anga ilizima mashambulio ya anga katika maeneo tofauti.

Shambulio hilo ni la hivi punde kutoka kwa Ukraine kutumia ndege zisizo na rubani zilizokuwa na silaha zinazolenga maeneo tofauti ya Urusi na eneo linalodhibitiwa na Moscow licha Kyiv kukanusha kuhusika na operesheni kama hizo.

Siku ya Ijumaa, maafisa wa Urusi walisema kwamba ndege zisizo na rubani za Ukraine zilidunguliwa zilipokuwa zikijaribu kushambulia Moscow - siku ya tatu mfululizo ya majaribio ya kushambulia mji mkuu wa Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.