Pata taarifa kuu

Ukraine yadai kudungua zaidi ya ndege kumi zisizo na rubani za Urusi

Zaidi ya ndege kumi zisizo na rubani za Urusi zilizolenga Kiev zilidunguliwa usiku wa Jumanne kjamkia Jumatano, na kusababisha vifusi kuyoanguka hali ambayo imeosababisha uharibifu wa mali lakini hakuna majeruhi, mamlaka imesema.

Vikosi vya jeshi la Ukraine vikikabiliana an amashambulizi ya Urusi.
Vikosi vya jeshi la Ukraine vikikabiliana an amashambulizi ya Urusi. REUTERS - VIACHESLAV RATYNSKYI
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na utawala wa kijeshi wa Kyiv, makundi ya ndege zisizo na rubani za "Shahed" zilizotengenezwa na Iran, zikitoka pande kadhaa, wakati huo huo zilipenya anga ya mji mkuu.

"Malengo yote - zaidi ya ndege kumi zisizo na rubani- yamegunduliwa na kuharibiwa kwa wakati," Serguii Popko, mkuu wa utawala wa kijeshi, amesema kwenye Telegram.

Mabaki ya ndege zisizo na rubani, hata hivyo, yameanguka kwenye vitongoji vya Solomyansky, Golosiivsky na Svyatoshynsky. "Kunaripotiwa hasara ya majengo yasiyo na wakazi na sehemu za barabara, bila uharibifu au moto mkubwa," utawala wa kijeshi umeongeza kwenye Telegram.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.