Pata taarifa kuu

Urusi inadai kuzima shambulio la ndege zisizo na rubani mjini Moscow

Kulingana na meya wa Moscow, shambulio la ndege zisizo na rubani kutoka Ukraine limelenga na kuharibu kidogo sehemu za mbele za minara miwili ya ofisi katika mji mkuu, bila kusababisha hasara yoyote.

Jumba refu lililoharibiwa na shambulio la ndege isiyo na rubani huko Moscow, Julai 30, 2023.
Jumba refu lililoharibiwa na shambulio la ndege isiyo na rubani huko Moscow, Julai 30, 2023. AP
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Moscow, Jean-Didier Revoin

Kulingana na mamlaka, ndege tatu zisizo na rubani zilidondoshwa usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili karibu saa tisa usiku huko Moscow. Ndege moja ilidunguliwa katika mkoa wa Moscow. Zingine mbili ziliangushwa na kuanguka kwenye eneo la Moscow-City, eneo la kibiashara la jiji ambapo pia kunapatikana majengo ya serikali.

Mamlaka inasema hili ni shambulio la tatu la ndege zisizo na rubani wiki hii. Mnamo Julai 24, ndege zisizo na rubani zilishambulia majengo mawili yasiyo ya makazi katika mji mkuu, na siku nne baadaye, mnamo Julai 28, meya wa jiji hilo Sergei Sobyanin alitangaza kwamba shambulio lilizimwa.

Kulingana na meya wa Moscow, shambulio la usiku huu lilisababisha uharibifu wa nyenzo bila kujeruhi watu. Limelenga eneo la kibiashara la jiji, Moscow-City, na hasa minara mikubwa ya vioo ambayo pia kunapatikana ofisi vitengo mbalimbali za Wizara za Fedha, Maendeleo ya Uchumi na Viwanda na Biashara. Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilishutumu "jaribio la shambulio la kigaidi".

Ndege zisizo na rubani ziliharibu sehemu ya mbele ya minara miwili katika eneo hili la kibiashara wakati zikidondoka, diwani wa jiji amesema kwenye Telegram. Ukumbi wa jiji pia umebainisha kwamba hakukuwa na waathiriwa au majeruhi, huku shirika la habari la TASS likisema kuwa mlinzi amejeruhiwa.

Hatimaye, shambulio hili limesababisha kufungwa kwa muda kwa uwanja wa ndege wa Vnukovo, magharibi mwa mji mkuu, ambapo shughuli za usafiri wa ndege zilielekezwa kwenye viwanja vya ndege vingine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.