Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Putin adai kusababisha hasara 'mbaya', Kyiv yadai 'kusonga mbele'

Vipi kuhusu siku za kwanza za mashambulizi ya Ukrainei dhidi ya wanajeshi wa Urusi? Hilo ni swali wengi wanajiuliza. Jumatatu jioni, rais wa Ukraine alikiri kwamba operesheni ilikuwa "ngumu" lakini akathibitisha kuwa wanajeshi wake wanaendelea kusonga mbele. Jumanne hii, Juni 13, rais wa Urusi alisema kinyume chake, akidai kuwa amelitimua jeshi la Ukraine. Lakini kwa kujibu, Kyiv na washirika wake wanadai kupata ushindi mwingine katika uwanja wa vita. 

Rais wa Urusi Vladimir Putin wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Kremlin, Moscow mnamo Juni 13.
Rais wa Urusi Vladimir Putin wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Kremlin, Moscow mnamo Juni 13. AP - Gavriil Grigorov
Matangazo ya kibiashara

Mbele ya kundi dogo la waandishi wa habari, Vladimir Putin amedai kuwa jeshi lake limepata ushindi mkubwa dhidi ya mashambulizi ya wanajeshi wa Ukraine hivi karibuni. Rais wa Urusi anatambua kushindwa kidogo katika mashambulizi hayo: ukosefu wa maandalizi mbele ya mashambulizi yaliyofanywa kwenye ardhi ya Urusi kutoka Ukraine au hata baadhi ya silaha ambazo zilishindwa kufanya kazi. Lakini linapokuja suala la kukabiliana na mashambulizi lililozinduliwa na Ukraine, anadai ushindi kamili. Katika siku chache, Ukraine ilikuwa tayari imepoteza "25% au 30%" ya vifaa vilivyotolewa na nchi za Magharibi, alisema rais wa Urusi.

"Siyo tu vifaru 160 viliharibiwa lakini pia magari 360 ya mapigano ya vikosi vya nchi kavu. Sio tu vifaa kutoka nchi za NATO. Pia kuna magari ya kivita ya Soviet. Lakini iwe ni vifaru aina ya Bradley au Leopards, vinaungua vizuri bila tatizo,” aliongeza rais wa Urusi. Kejeli hizo zinalenga silaha za Marekani na Ujerumani zilizotumwa nchini Ukraine. Na ili kuibua hoja hiyo, rais wa Urusi anakejeli kuhusu muda huo wa kukabiliana na mashambulizi, wakati Ukraine imekuwa ikitayarisha shambulio hili kwa miezi kadhaa.

Katika ziara yake mjini Washington, Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, aliema kuwa uungwaji mkono wa nchi wanachama wa Muungano wa Ukraine unazaa matunda. "Msaada ambao tunatoa kwa pamoja kwa Ukraine sasa unaleta mabadiliko kwenye uwanja wa vita hivi sasa, kwa sababu mashambulizi yanaendelea na wanajsi wa Ukraine wanapiga hatua, na wanafanya vizuri kwenye uwanja wa vita. Bado ni mapema,” alisema. Kamanda Mkuu wa jeshi la Ukraine, kwa upande wake, alithibitisha kwamba operesheni zinaendelea kulingana na mpango na kwamba jeshi la Ukraine linasonga mbele.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.