Pata taarifa kuu

Urusi yadai kuzuia jaribio la uvamizi kutoka Ukraine katika jimbo la Belgorod

Mashambulizi kutoka Ukraine katika eneo la Belgorod, inaonekana, yamefikia kiwango kikubwa zaidi. Mada hiyo inagonga vichwa vya habari kwenye runinga za Urusi. Kremlin inahakikishia: Wizara ya Ulinzi, idara ya mpaka ya FSB, Wizara ya Hali ya Dharura na mamlaka ya kikanda wanawasiliana mara kwa mara na Vladimir Putin. Wahalifu walikuwa sawa na wale ambao walidhibiti sehemu ya jimbo la Urusi kwa saa 36 siku tisa zilizopita.

Magari yaliyoharibiwa katika mji wa Shebekino katika jimbo la Belgorod, Urusi, kwen,ye picha hii iliyotolewa Mei 31, 2023.
Magari yaliyoharibiwa katika mji wa Shebekino katika jimbo la Belgorod, Urusi, kwen,ye picha hii iliyotolewa Mei 31, 2023. via REUTERS - GOVERNOR OF BELGOROD REGION
Matangazo ya kibiashara

Kutoka kwa mwandishi wetu huko Moscow,

Mji wa Shebekino, umekuwa chini ya "mashambulizi makubwa" tangu Jumatano, Mei 31, mamlaka ya eneo hilo imesema.

Mashambulizi haya yamesababisha uharibifu mkubwa: paa za majengo katikati ya jiji zikiwa zimeungua, Roketi za Grad zikirushwa kwenye mtambo wa ndani wa Wizara ya Mambo ya Ndani, umeme umekata, huku kukiletwa mabasi kwa minajili ya kuwahamisha raia, watoto na akina mama kwanza.

Shebekino, mji wenye wakazi 40,000, sasa umekaribia kuwa tupu. Kwa mujibu wa ushuhuda kwenye televisheni ya Urusi, hakuna kitu kinachofanya kazi tena katika jiji hili la ambalo kila mtu anajua nchini Urusi, kwa kuwa ni makao ya moja ya viwanda vya pasta vya bei nafuu na vinavyouzwa zaidi. Unaweza kuzipata kwenye rafu zote za maduka makubwa.

Jeshi la Urusi linadai kutumia wanajshi wa nchi kavu na anga kukabiliana na mashambulizi matatu yaliyoratibiwa na "wahujumu": sawa na wale ambao walikuwa wamedhibiti sehemu ya jimbo la Belgorod siku 9 zilizopita.

Kulingana na vituo kadhaa vya Telegraph, wapiganaji hawa walikuwa wakisafiri kwenye magari mepesi ya kivita. Idadi rasmi ya kwanza inaonyesha watu wachache tu waliojeruhiwa na hakuna vifo. Washambuliaji thelathini, kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Urusi, waliuawa.

Kremlin inalaani ukimya kutoka jumuiya ay kimataifa kwa kutokosoa hali hiyokimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.