Pata taarifa kuu

Urusi: Belgorod yakumbwa na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani

Jimbo la Belgorod nchini Urusi limelengwa na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani usiku wa Jumatatu Mei 22 kuamkia Jumanne Mei 23, baada ya kuvamiwa na wapiganaji ambao walizua 'wasiwasi mkubwa' kwa msemaji wa Vladimir Putin huko Moscow.

Rais wa Urusi Vladimir Putin, Machi 24, 2023.
Rais wa Urusi Vladimir Putin, Machi 24, 2023. AP - Alexei Babushkin
Matangazo ya kibiashara

Uvamizi wa wapiganaji wenye silaha kutoka Ukraine ulisababisha takriban watu wanane kujeruhiwa na kupelekea Urusi kutangaza sheria ya kupambana na ugaidi katika eneo hilo. Shambulio hili, kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa tangu mwanzo wa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, limedaiwa na makundi mawili ya wapiganaji ambao wanapigana kwa kuisaidia Ukraine. Je, makundi haya yana uwezo gani na sababu za mashambulizi yao ?

Kuna mkundi mawili ambayo yamedai uvamizi huu: Jeshi la Uhuru kwa Urusi na Jeshi la Kujitolea la Urusi. Kundi la kwanza linaundwa na vikosi kadhaa vya watu wanaojitolea, wapiganaji elfu kwa jumla; kundi hili lilianzishwa mwanzoni mwa vita, nembo yake ni ngumi iliyokunjwa iliyofunikwa na maneno "Uhuru" na "Urusi", na lengo lake ni kurudisha ukubwa asilia wa Urusi, lakini bila Vladimir Putin, anayechukuliwa kuwa kiongozi fisadi , asiyefaa na asiye waaminifu.

Kyiv yakaribisha mashambulizi Belgorod

Kundi lingine, Kikosi cha Kujitolea cha Urusi, kinaundwa na wazalendo, Wanazi mamboleo wa zamani - ambao baadhi yao walifika Ukraine muda mrefu kabla ya vita kwa sababu waliogopa kukamatwa kwa uhuni. Lengo lao pia ni kumpindua Vladimir Putin, lakini hasa kwa sababu machoni pao Putin halitetei taifa la Urusi kutoka kwa mtazamo wa kikabila. Sehemu ndogo ya kiitikadi, lakini lengo lile lile: kuleta vita kwa Urusi ili, mwishowe, kupindua nguvu za kijeshi za Urusi.

Makundi yote hayo yanasema kwamba ikiwa Ukraine itashinda Urusi, wataendelea kupigania lengo hilo. Hadi sasa, makundi haya mawili yalikuwa hayajaratibu, hii ni mara ya kwanza kwa kutekeleza mashambulio pamoja, hatua iliyokaribishwa huko Kiev na Ilya Ponomarev, mbunge wa zamani wa Buge la Urusi (Duma) ambaye amekuwa akijaribu tangu kuanza kwa vita kujumuisha kisiasa upinzani huu wa kijeshi dhidi ya Vladimir Putin.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.