Pata taarifa kuu

Vita vya Ukraine vyatimiza mwaka mmoja

Siku ya Alhamisi Februari 24, 2022, Rais wa Urusi Vladimir Putin alianzisha mashambulizi dhidi ya Ukraine, na kutikisa bara zima la Ulaya. Mwaka mmoja baadaye, RFI inaangazia kipindi chote hiki cha vita, sababu na madhara yake.

Mwaka mmoja uliopita, mnamo Februari 24, 2022, Urusi ilianzisha mashambulizi dhidi ya Ukraine.
Mwaka mmoja uliopita, mnamo Februari 24, 2022, Urusi ilianzisha mashambulizi dhidi ya Ukraine. © AP / Montage FMM
Matangazo ya kibiashara

Ni siku 365 zimepita, ambapo Waukraine waliamshwa kwa milio ya risasi milipuko ya mabomu. Siku ya Alhamisi Februari 24, 2022, muda mfupi kabla ya saa kumi usiku za Afrika Mashariki, Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema maneno haya katika hotuba rasmi ya televisheni: “Nimeamua kutekeleza operesheni maalum ya kijeshi” nchini Ukraine. Akibaini kwama lengo ilikuwa, "kudhoofisha kijeshi na kuvunja itikadi za kinazi" kwa nchi jirani. Kisha, akiwalenga moja kwa moja askari wa Ukraine, Vladimir Putin aliwataka "waweke chini silaha zao".

Kwa wiki kadhaa, ujasusi wa nchi za Magharibi uliionya juu ya harakati za wanajeshi wa Urusi kwenye mpaka na Ukraine. Ni kufuatia hali hii ambapo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana wakati Vladimir Putin alizungumza. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, kisha alitoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mzozo huo. Balozi wa Ufaransa, Nicolas de Rivière, kwa upande wake, alishutumu "dharau" iliyoonyeshwa na Urusi kwa Umoja wa Mataifa.

Mashambulizi ya mara kwa mara

Wakati huohuo, karibu sa kumi na nusu usiku, milipuko ilisikika katikati ya mji wa Kyiv na katika miji kadhaa ya mashariki mwa nchi, hasa huko Mariupol. Asubuhi na mapema, kamera za uchunguzi zilinasa vivaru vya Urusi kwenye mpaka. Wakati huo huo Ukraine ilitangaza kuwa imedungua ndege na helikopta za Urusi, huku jeshi la Urusi lilidai kuharibu mifumo ya ulinzi ya anga ya Urusi na kulenga tu maeneo yao ya kijeshi. Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, Vassily Nebenzia, alihakikisha mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa: "Hatujafanya chokochoko dhidi ya raia wa Ukraine, lakini kwa kundi linalotawala huko Kiev. »

Baada ya saa chache, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alitangaza kuchukua nafasi ya kiongozi wa kijeshi na kushangaza ulimwengu wote kwa harakati zake. Pao hapo alivunja uhusiano wake wa kidiplomasia na Moscow, na kutangaza sheria ya kijeshi na kuagiza uhamasishaji wa jumla. "Msiogope, tutashinda," alisisitiza katika hotuba kwa taifa mwanzoni mwa mashambulizi, ya kwanza katika mfululizo mrefu wa hotuba zake.

Saa moja asubuhi. Karibu na Kharkiv, mji ulioko kaskazini-mashariki pia ulilengwa na mashambulizi makubwa ya mabomu, majeshi ya nchi hizo yalianza kukabiliana. Katika mji mkuu, umati wa raia wa Ukraine walikimbilia kwenye njia za chini ya ardhi, kujikinga na mabomu au kujaribu kuondoka mji huo. Msongamano wa magari ulionekana kwenye barabara za kutoka mjini. "Vituo vya mafuta vilivamiwa na madereva. Misururu mirefu ilionekana kwenye barabara inayounganisha Mariupol na Zaporijgia,” alisema mwanahabari wetu maalum, Anastasia Bechio, siku hiyo.

Hasira ya kimataifa

Alhamisi, Februari 24, 2022 , vituo vya habari duniani vilirusha picha za mashambulizi ya anga ya Urusi katika miji ya Ukraine. Siku nzima, maelfu ya waandamanaji waliandamana katika nchi nyingi kupinga uvamizi wa Urusi. Wakati huo huo, Urusi ilitangaza kwamba inadhibiti maeno kadhaa katika jimbo la Donbass, upande wa mashariki, wakati raia wa kwanza wa Ukraine wakikimbilia Poland au Moldova. Karibu saa kumi alaasiri, uwanja wa ndege wa kijeshi wa Hostomel, kaskazini mwa Kyiv, ulianguka mikononi mwa jeshi la Urusi. Baadaye kidogo, ilikuwa zamu ya kituo cha nishati cha Chernobyl kudhibitiwa na Urusi. Hata hivyo jeshi la Ukraineliliedelea kukabiliana na mashambulizi ya Urusi.

Wakati mapigano yakiendelea na vikosi vya ardhini vya Urusi kuingia nchini Ukraine, NATO ililaani "shambulio la kijinga" la Kremlin, Rais wa Marekani Joe Biden alithibitisha kwamba "ulimwengu utadai uwajibikaji wa Urusi". Wakuu wengi wa nchi kote ulimwenguni walikasirishwa na kitendo hiki cha Urusi na kutangaza msaada wao kwa Ukraine. Emmanuel Macron alibaini kwamba kumetokea "mabadiliko katika historia ya Ulaya" huku akihakikisha: "Hatutakuwa na udhaifu na tutajibu kwa utulivu. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.