Pata taarifa kuu

Harakati za Wagner barani Afrika vita ya Ukraine ikitimiza mwaka mmoja

NAIROBI – Wakati huu vita ya Ukraine, ikitimiza mwaka mmoja tangu ianze, idadi ya wapiganaji mamluki imeendelea kuongezeka barani Afrika, na kwasasa kundi maarufu ni lile la Urusi linalofahamika kama Wagner, ambalo lina wanajeshi na pia maslahi ya kibiashara.Katika kuadhimisha mwaka mmoja tangu Urusi ivamie Ukraine, mwandishi wetu Emmanuel Makundi, analiangazia kwa kina kundi hili na shughuli zake barani Afrika…

Ni mwaka mmoja sasa tangu Urusi ilipoivamia Ukraine
Ni mwaka mmoja sasa tangu Urusi ilipoivamia Ukraine AP - Emilio Morenatti
Matangazo ya kibiashara

Kwasasa kundi hili linawapiganaji kwenye nchi za Mali, Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Msumbiji na Libya, ambapo wanashirikiana na ama wanajeshi wa Serikali au makamanda wa makundi yenye silaha na kulipwa fedha taslimu au mali kama vile madini na mafuta.

Hata hivyo tangu uwepo wake kwenye nchi hizi, wapiganaji wake wananyooshewa  kidole kwa kutekeleza vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu.

Kundi la Wagner, halipigani tu vita kwaajili ya kupata dhahabu, ila kupitia mtandao wake wa makampuni ya mafuta, limekuwa msaada mkubwa kwa utawala wa Kremlin ambao unazisaidia nchi kadhaa za Afika, ambapo limekuwa likijihusisha na siasa, kuwalinda watawala wa kiimla na kufanya propaganda.

Licha ya ushahidi uliopo kuonesha kundi hili lina baraka na mkono wa rais Vladmir Putin, ambapo Serikali imekuwa ikiliwezesha kwa silaha za kivita nchini Ukraine na hata barani Afrika, utawala wa Moscow unakanusha kuwa na uhusiano wowote,

Mwaka 2017 kundi hili lilianza kusambaa barani Afrika, likiwashauri watawala wa kimabavu, kueneza propaganda na hata kutuma waangalizi wa kughushi wa uchaguzi kwenye mataifa kadhaa ya Afrika, imeonesha ripoti ya umoja wa Mataifa.

Katika eneo la Afrika Magharibi, kundi hili linatumia mwanya wa kampeni hasi dhidi ya Ufaransa, hasa nchini Mali, ambapo kuwasili kwa wapiganaji wa Wagner kulisababisha ufaransa kuondoa wanajeshi wake na kutatizika kwa uhusiano wa kidiplomasia, huku hofu kama hii ikishuhudiwa Burkina Faso ambako nako Ufaransa imeondoa wanajeshi wake.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.