Pata taarifa kuu

'Makubaliano' yaliyotangazwa na Vladimir Putin nchini Ukraine hayakufanyika

Vladimir Putin alihakikisha kwamba jeshi la Urusi litatekeleza "usitishwaji mapigano" wa saa 36 wakati wa Krismasi ya Orthodox, Januari 7. Hata hivyo, mapigano yaliendelea pande zote mbili siku ya Ijumaa na Jumamosi, na jeshi la Urusi liliendelea kushambulia Ukraine.

Moshi mwingi unaongezeka katika eneo la Bakhmout mnamo Januari 7, 2023, baada ya mashambulizi ya angani ya Urusi wakati wa kusitishwa kwa mapigano kwa saa 36 na mpango uliotangazwa na Rais wa Urusi kwa kusheherekea Krismasi ya Kiorthodoksi.
Moshi mwingi unaongezeka katika eneo la Bakhmout mnamo Januari 7, 2023, baada ya mashambulizi ya angani ya Urusi wakati wa kusitishwa kwa mapigano kwa saa 36 na mpango uliotangazwa na Rais wa Urusi kwa kusheherekea Krismasi ya Kiorthodoksi. © REUTERS - CLODAGH KILCOYNE
Matangazo ya kibiashara

Mara tu Vladimir Putin alipopendekeza siku ya Alhamisi, Januari 5, viongozi wa Kyiv waliuita mpango huo kuwa mtego wa kijinga na mbinu ya kuchelewesha. Kwa upande wa Ukraine, kwa hivyo hakukuwa na suala la kusitisha mapigano na Kyiv haijawahi kujitolea kufanya usitishaji mapigano.

Hasa tangu Ijumaa mchana, wanajrshi wa Urusi hawajaweka chini slaha. Siku ya Ijumaa na Jumamosi kuliripotiwa mashambulizi ya angani ya Urusi katika majimbo ya  Kherson, Kramatorsk, Zaporizhia na Chernihiv. Na mapigano makali yamekuwa yakiendelea kwa saa 48 katika eneo la Soledar, nje kidogo ya Bakhmout, huko Donbass.

Kwa wiki nzima, vikosi vya Urusi, na hasa wanamgambo wa Wagner, walijaribu kudhibiti eneo la Soledar, hasa wakati wa mchana, wakati vikosi maalum na askari wa miavuli wa Ukraine walionekana kushambulia usiku na kurejesha sehemu hizi kwenye hiomaya yapo.

Ujanja wa kisiasa

Mahali pengine, kunaweza kuwa na aina fulani ya hali ya mapigano, iliyohusishwa na tarehe hii ya mfano ya Krismasi, lakini katika maeneo kunakoripotiwa operesheni za kijeshi, hakukuwa na usitishaji wa mapigano.

Katika siku hizi, Kremlin inajaribu kutoa mwelekeo wa kidini kwenye vita. Wazo ni rahisi: kwa kutangaza "makubaliano" haya, Vladimir Putin alijifanya kama mtu mwenye nia njema, na hivyo kumuwezesha kuishtaki Kyiv kwa kuharibu Ukraine kama kikwazo cha amani , huku akionekana kama mlinzi wa Wakristo wa Orthodox. .

Lakini katika hali halisi, lengo la Kremlin halibadiliki hata kidogo, daima ni kulazimisha kyiv kukubali kujisalimisha, kwa masharti ya Moscow.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.