Pata taarifa kuu
ULINZI-DIPLOMASIA

Marekani kutoa dola bilioni 3 za msaada wa kijeshi kwa Ukraine

Marekani itatoa dola bilioni tatu kama msaada mpya wa kijeshi kwa Ukraine, ambao utajumuisha magari ya kivita aina ya Bradley, Ikulu ya White House imetangaza siku ya Ijumaa.

Kifaru cha Ujerumani Marder (kushoto) na kifaru cha Marekani Bradley (kulia).
Kifaru cha Ujerumani Marder (kushoto) na kifaru cha Marekani Bradley (kulia). © RFI via AP
Matangazo ya kibiashara

Msaada huu, ambao maelezo yake yatatolewa na Pentagon baadaye, pia utajumuishe magari ya kivita yatakayowasafirisha wanajeshi wenye silaha aina ya Howitzers, msemaji wa Ikulu ya White House Karine Jean-Pierre amesema.

Washington na Berlin walitangaza siku ya Alhamisi kwamba wataipa Kyiv magari ya kivita, wa aina ya Bradley upande wa Marekani na wa aina ya Marder upande wa Ujerumani, lakini hawakuonyesha aina hizo za magari. Vifaru aina ya Marder ambavyo vinafanya kazi tangu miaka ya 1970,  ni magari mepesi ya kivita yaliyokusudiwa usafirishaji wa askari.

Bradleys ni magari ya kivita ya aina moja na hayo ya Ujerumani, ambayo yanafanya kazi tangu mwanzo wa miaka ya 1980. 

"Tuna hakika kwamba hii itasaidia (vikosi vya Ukraine) kwenye uwanja wa vita," ameongeza Karine Jean-Pierre.

DRC: Wanaharakati wana mashaka na ahadi za M23 kuondika Rumangabo

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, waasi wa M 23 wanatarajiwa kuondoka na kukabidhi Rumangabo, kambi kubwa ya wanajeshi wa DRC kwa vikosi vya Jumuiya ya Afrika Mashariki, baada ya kuahidi kuondoka. 

Waharakati wanasema hawaamini iwapo waasi hao wataondoka kabisa katika eneo hilo la  kambi ya Rumangambo, baada ya kuondoka kwao mjini Kibumba kutiliwa shaka na jeshi la DRC, kama anavyoeleza HENRI MAHANO, kiongozi wa Shirika la kirai katika eneo hilo. 

Wakati hili likitarajiwa, ripoti zinasema jana; waasi hao waliendelea kusonga mbele katika Wilaya ya Rutshuru na kuchukua eneo la Nyamilima. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.