Pata taarifa kuu

Ufaransa kuipa Ukraine vifaru vyepesi kukabiliana na uvamizi wa Urusi

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemtangazia mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky Jumatano kwamba Ufaransa itaipa Ukraine 'vifaru vyepesi vya vita' vilivyotengenezwa nchini Ufaransa, kulingana na taarifa kutoka Ikulu ya ElysΓ©e.

Wanajeshi wa Ufaransa wakiwa katika kifaru cha kivita aina ya AMX-10 RC, huko Villepinte, kitongoji cha kaskazini mwa Paris, Juni 12, 2022.
Wanajeshi wa Ufaransa wakiwa katika kifaru cha kivita aina ya AMX-10 RC, huko Villepinte, kitongoji cha kaskazini mwa Paris, Juni 12, 2022. AFP - EMMANUEL DUNAND
Matangazo ya kibiashara

"Rais ametaka kuongeza" misaada hii ya kijeshi ambayo tayari imetolewa kwa Kyiv "kwa kukubali kutoa vifaru vyepesi aina ya AMX-10 RC", imesema ikulu ya rais wa Ufaransa. "Hii ni mara ya kwanza kwa vifaru vilivyoundwa na nchi za Magharibi kutolewa kwa wanajeshi wa Ukraine," amesema baada ya mazungumzo ya simu ya saa moja kati ya viongozi hao wawili.

Kulingana na Paris, Emmanuel Macron, ambaye amethibitisha tena kwa Volodymyr Zelensky "msaada usio kuwa na shaka" wa Ufaransa "hadi ushindi", hivyo ametaka "kuonyesha uimara na mwendelezo" wa msaada wa kijeshi wa Ufaransa.

AMX-10 RC ni vifaru vyepesi ambavyo hutembea kwa matairi na sio kwa minyororo, " na imekubaliwa kuwa ni vifaru vya zamani lakini vyenye nguvu", amesema mshauri wa masuala ya kijeshi katika Jeshi la Ufaransa, mfumo huu utabadilishwa hatua kwa hatua na Jaguar kuchukuwa nafasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.