Pata taarifa kuu
URUSI- UKRAINE MAPIGANO

Ukraine na Umoja wa Ulaya kufanya kikao mjini Kyiv mwezi Februari

Ofisi ya rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky,imesema taifa lake na umoja wa Ulaya EU watakuwa na mkutano mjini Kyiv tarehe 3 ya mwezi Februari mwaka huu.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na rais wa tume ya umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen,11 juni 2022.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na rais wa tume ya umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen,11 juni 2022. AFP - SERGEI SUPINSKY
Matangazo ya kibiashara

Tangazo la Kyiv linakuja wakati huu rais Zelensky akisema Moscow inapanga kuishambulia nchi yake kwa makombora ya ndege zisizo na rubani kama njia moja ya kuwashusha wanajeshi wake morale ya kupamabana na wanajeshi wa Urusi.

Haya yanajiri wakati huu pia  jeshi la Urusi likidhibitisha kuauwa kwa wanajeshi wake 60 katika shambulio la Ukraine Mashariki mwa eneo la Donbas.

Ukraine kwa upande wake imendelea kusisitiza iliwauua wanajeshi 400 wa Urusi katika shambulio hilo la mkesha wa mwaka mpya wa 2023.

Shambulio hilo limezua ghadhabu kutoka kwa raia wa Moscow pamoja na baadhi ya wabunge wanaowataka makamanda wa jeshi la Urusi kuadhibishwa kwa kupuuza atahri za kutokea kwa shambulio hilo.

Katika hotuba ya mwaka mpya kwa raia wake,marais wa Urusi na Ukraine wote waliahidi kupata ushindi katika mapigano mwaka huu mwa 2023.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.