Pata taarifa kuu
URUSI- UKRAINE MAPIGANO

Ukraine inasema imewauwa wanajeshi wa Urusi katika shambulio la kombora

Ukraine inasema imewauwa karibia wanajeshi 400 wa Urusi katika shambulio la kombora kwenye eneo linalokaliwa na wanajeshi wa Urusi la Donetsk.

Wanajeshi wa Ukraine
Wanajeshi wa Ukraine REUTERS - CLODAGH KILCOYNE
Matangazo ya kibiashara

Kombora hilo lililenga jengo moja katika mji wa Makiivka, ambapo maofisa wa jeshi la Urusi inadhaniwa walikwepo wakati wa shambulio hilo.

Idadi ya wanajeshi hao wa Urusi wanaodiwa kuawaua na jeshi la Ukraine haijaekwa wazi ila mamlaka zinazounga mkono Urusi zimedhibitisha kuwepo kwa majeruhi, lakini hazikuthibitisha idadi ya waliouawa.

Taarifa ya Ukraine inakuja wakati huu ambapo Urusi imeendelea kutekeleza mashambulio ya ndege zisizo na rubani katika maeneo tofauti nchini Ukraine.

Daniil Bezsonov, afisa mkuu anayeungwa mkono na Moscow katika maeneo yanayokaliwa na Urusi ya Donetsk,amedhibitisha tukio la usiku wa kuamkia mwaka mpya.

Baadhi ya wachambuzi wa Urusi na wanablogu wamekiri kutokea kwa shambulio hilo  japokuwa wanasema idadi ya waliouawa ni  ndogo kuliko ilivyodaiwa na Ukraine.

Jeshi la Ukraine limesema watu 300 walijeruhiwa katika shambulio hilo la kombora watu wengine 400 wakiripotiwa kuawaua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.