Volodymyr Zelensky apuuzia mbali wito wa kusitisha vita wa Urusi
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, amepuuzia wito wa mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, ambaye ametangaza usitishwaji wa vita, wakati dhehebu la Orthodox linapoadhimisha sikukuu ya Krismasi.
Imechapishwa:
Rais Zelenskyy, amesema tangazo la Putin, ni mbinu ya kurudisha nyuma jitihada za jeshi la Ukraine, kuendelea kulikomboa jimbo la Donbasa, Mashariki mwa nchi yake na Urusi inataka kutumia fursa hiyo kuwaingiza zaidi wanajeshi wake nchini Ukraine.
Aidha, Ukraine inasema vita vitaisha iwapo Urusi itaondoa wanajeshi wake, katika ardhi yake. Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guteress amesema anakaribisha usitishwaji wowote wa kusitisha vita, katika sikukuu ya Krismasi, licha ya kwamba hatua hiyo haiwezi kumaliza vita vinavyoendelea.
Siku ya Alhamisi, rais Putin alitangaza kuwa jeshi lake halitaendeleza vita kwa saa 36, kuanzia saa tatu asubuhi, saa za Kimataifa mpaka siku ya Jumamos saa tatu usiku, ili kutoa nafasi kwa waumini wa dhehebu la Orthodox nchini Urusi kusherehekea krismasi siku ya Jumamosi.