Pata taarifa kuu

Urusi yapeleka makombora ya kutungulia ndege Moscow

Siku ya Ijumaa Januari 20, watumiaji wa Intaneti wa Urusi walirusha hewani video kadhaa zinazoonyesha mifumo ya makombora ya ulinzi wa anga ya Pantsir imewekwa katika maeneo tofauti katika mji mkuu wa Urusi, ikiwa ni mbali sana na maeneo ya vita na sehemu ya mbele isiyoweza kufikiwa na jeshi la Ukraine.

Video ya jeshi la Urusi inayoonyesha betri ya mifumo ya kuzuia ndege ya S-400 zikielekeza makombora yake angani kutoka eneo lenye theluji katika eneo la Belarus la Brest, linalopakana na Ukraine, mnamo Februari 2022.
le 10 février 2022
Video ya jeshi la Urusi inayoonyesha betri ya mifumo ya kuzuia ndege ya S-400 zikielekeza makombora yake angani kutoka eneo lenye theluji katika eneo la Belarus la Brest, linalopakana na Ukraine, mnamo Februari 2022. le 10 février 2022 © ARMÉE RUSSE, VIA AGENCE FRANCE-PRESSE
Matangazo ya kibiashara

Katika picha zinazozunguka kwenye mitandao ya kijamii ya Kirusi, kunaonekana makombora ya kutungulia ndege chini ya kumi na mbili huko Moscow, ikiwa ni pamoja na moja iliyowekwa kwenye paa la Wizara ya Ulinzi, katikati ya jiji. Betri nyingine iliripotiwa kutumwa takriban kilomita kumi kutoka kwa makazi ya Vladimir Putin huko Novo-Ogariovo, magharibi mwa Moscow.

Uvumi umejaa sababu ya kupelekwa kwa mifumo hii ya kisasa zaidi, hasa kwani Kremlin inakataa kutoa maoni, na mjumbe wa Bunge la Urusi anazungumza, licha ya ushahidi, kuwa ni "habazi za uongo" na " picha zilizotengenzwa".

Lipi lengo la Moscow?

Baadhi ya wataalam wanasema, ni lazima juu ya yote kuonekana kama operesheni ya kisaikolojia, hali ya kuwatia uoga raia Urusi, kuwafanya wahisi kuwa wako katika hali ya vita.

Wengine wanasema, ikiwa makombora haya yatatumwa, ni kwa sababu Kremlin haina uhakika tena wa kutoweza kuathirika kwa mji mkuu wake. Katika miezi ya hivi karibuni, kambi za wanajeshi wa anga wa Urusi, wakati mwingine mbali maeneo ya vita, zilishambuliwa na ndege zisizo a rubani za masafa marefu za Ukraine. Hakuna anayejua kuhusu ndege hizi mpya zisizokuwa na rubani, lakini ni wazi, kwa upande wa Urusi, zinachukuliwa kwa kwa umakini.

Kwa vyovyote vile, Urusi imetangaza siku y Jumamosi Januari 21 kwamba imefanya mazoezi ya ulinzi wa anga katika mkoa wa Moscow, ili kulinda miundombinu yake muhimu katika tukio la "mashambulizi ya anga", dhidi ya historia ya mzozo na Ukraine. "Mazoezi yamefanyika katika mkoa wa Moscow, pamoja na wafanyakazi wa kikosi cha mlakombora ya kuzuia ndege cha Wilaya ya Kijeshi ya Magharibi, ili kurudisha nyuma mashambulio ya anga dhidi ya miundombinu muhimu ya kijeshi, viwanda na kiutawala," Wizara ya Usalama ya Urusi imesema katika taarifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.