Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-ULINZI

Ujerumani: Hakuna uamuzi juu ya kuipa Ukraine vifaru aina ya Leopard

Hakuna uamuzi wowote kufikia sasa ambao umetolewa katika juu ya uwezekano wa kuipa Kyiv ya vifaru aina ya Leopard, vilivyotengenezwa na Ujerumani, ambavyo Ukraine inahitaji kuzima uvamizi wa Urusi, waziri mpya wa ulinzi wa Ujerumani amesema Ijumaa.

"Hatuwezi kusema leo ni lini (uamuzi utatolewa) na uamuzi utakuwa upi kwenye vifaru vya Leopard," amesemaBoris Pistorius, Waziri mpya wa ulinzi wa Ujerumani. Washirika wa Ukraine wanakutana katika kambi ya anga ya Marekani ya Ramstein siku ya Ijumaa ili kuamua juu ya msaada wa ziada wa kijeshi kwa Kyiv.
"Hatuwezi kusema leo ni lini (uamuzi utatolewa) na uamuzi utakuwa upi kwenye vifaru vya Leopard," amesemaBoris Pistorius, Waziri mpya wa ulinzi wa Ujerumani. Washirika wa Ukraine wanakutana katika kambi ya anga ya Marekani ya Ramstein siku ya Ijumaa ili kuamua juu ya msaada wa ziada wa kijeshi kwa Kyiv. © REUTERS / RADOVAN STOKLASA
Matangazo ya kibiashara

Suala hilo "limejadiliwa" kati ya washirika wa Ukraine waliokutana mjini Ramstein, magharibi mwa Ujerumani, lakini "hakuna uamuzi uliochukuliwa", Boris Pistorius ameuambia mkutano na waandishi wa habari.

"Hatuwezi kusema leo ni lini (uamuzi utatolewa) na uamuzi utakuwa upi kwenye vifaru aina ya Leopard," amesema. Washirika wa Ukraine wanakutana katika kambi ya anga ya Marekani ya Ramstein siku ya Ijumaa ili kuamua juu ya msaada wa ziada wa kijeshi kwa Kyiv.

Waziri huyo amedai kwamba "hisia" kwamba Ujerumani pekee inapinga kyiv kupewa vifaru ni "uongo". "Washirika wengi wanapeana maoni" ya Berlin, amemhakikishia waziri, akiamini kwamba "kuna sababu nzuri za kuwa na sababu nzuri za kupinga utoaji huu".

Ujerumani iko chini ya shinikizo kubwa kuidhinisha Ukraine kupewa vifaru vya Leopard 2 vilivyotengenezwa Ujerumani.

Poland na Finland zimeonyesha kuwa ziko tayari kusambaza aina hii ya vifaru kwa jeshi la Ukraine, lakini zinahitaji makubaliano kutoka Ujerumani, ambayo ilitengeneza vifaru hivyo.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zekensky siku ya Ijumaa alizitaka nchi za Magharibi kuharakisha uwasilishaji wa silaha nzito, ikiwa ni pamoja na vifaru na makombora ya masafa marefu, ili kuisaidia nchi yake katika vita muhimu vinavyokuja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.