Pata taarifa kuu

Msaada wa kijeshi kwa Ukraine: Washirika kujadili mkakati mpya dhidi ya uvamizi wa Urusi

Volodymyr Zelensky alisema Alhamisi kwamba Ukraine inatarajia maamuzi madhubuti mwishoni mwa mkutano huu, wa 3 kati ya washirika wa Kyiv katika kambi ya Marekani huko Ramstein, magharibi mwa Ujerumani. Ukraine ambayo, kwa wiki nyingi, imekuwa ikitoa wito kwa mifumo ya makombora ya masafa marefu, lakini pia mizinga. Na swali hili, kwa usahihi, linagawanya viongozi wa nchi za Magharibi. Ujerumani, nchi mwenyeji wa mkutano huo, iko chini ya shinikizo haswa.

Kifaru cha aina ya Leopard 2 ikishiriki katika luteka ya kijeshi huko Letzlingen, Ujerumani, Machi 2011.
Kifaru cha aina ya Leopard 2 ikishiriki katika luteka ya kijeshi huko Letzlingen, Ujerumani, Machi 2011. Sean Gallup/Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Hakika ni Waziri mpya wa Ulinzi, Boris Pistorius, ambaye ataongoza ujumbe wa Ujerumani, mtaalamu wa masuala ya usalama wa ndani, na si katika jeshi. Zaidi ya yote, amekuwa akihudumu tangu Januari 19; kwa maneno mengine, nafasi yake ya majukumu itakuwa finyu, anaripoti mwandishi wetu wa mjini Berlin, Nathalie Versieux.

Pistorius atatekeleza maagizo ambayo amepokea kutoka kwa kansela. 

Ujerumani inakabiliwa na shinikizo kubwa linaloongezeka la kuitaka ipeleke vifaru vya kivita chapa Leopard nambari 2 nchini Ukraine. Rais Volodymyr Zelensky na viongozi wengine wameikosoa serikali ya Ujerumani kwa kujizuia kuipatia Ukraine silaha nzito nzito za ziada.

Akizungumzia yatakayojadiliwa leo waziri wa ulinzi wa Ujerumani amesisitiza Marekani ni mshirika muhimu wa Ujerumani. 

Pistorius atakutana na waziri mwenzake wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin katika kambi ya kijeshi ya Marekani ya Ramstein hapa Ujerumani kujadili suala la kuipelekea silaha zaidi Ukraine. 

Siku ay alhamisi Pistorius aliweka wazi kwamba nchi yake itachukua hatua kwa ushirikiano na Marekani. Hata hivyo Marekani inaiunga mkono Ujerumani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.