Pata taarifa kuu

Watu wengi wafariki akiwemo waziri mmoja katika ajali ya helikopta nchini Ukraine

Helikopta imeanguka Jumatano asubuhi karibu na shule ya chekechea katika mkoa wa Kyiv, na kuua  watu18 akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani Denys Monastyrsky na watoto watatu, janga jipya nchini Ukraine siku chache baada ya shambulio baya la Urusi huko Dnipro.

Mabaki ya helikopta iliyochanganyika na uchafu, karibu na gari lililoharibiwa.
Mabaki ya helikopta iliyochanganyika na uchafu, karibu na gari lililoharibiwa. © Національна поліція України
Matangazo ya kibiashara

" Ni msiba na huzuni huko Brovary. Idadi ya wahanga imeongezeka. Saa 10:30,  watu 18 walfariki dunia wakiwemo watoto 3," amesema gavana wa mkoa huo, Oleksiï Kouleba, kwenye Telegram. Amesema kuwa "pia kuna majeruhi 29, ikiwa ni pamoja na watoto 15", na kuongeza hofu ya kuwepo na idadi kubwa zaidi ya waathiriwa.

Kwenye picha zinazozunguka kwenye mitandao ya kijamii, kunaonekana mabaki ya helikopta hiyo yakiwa yamechanganyikana na uchafu, karibu na gari lililoharibiwa vibaya. Maafisa wa idara ya Zima moto na polisi walikuwa kwenye eneo la tukio, kulingana na timu ya shirika la habari la AFP.

Miongoni mwa waathiriwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani Denys Monastyrsky, 42, naibu wake wa kwanza Yevgeny Yenine, na katibu wa Waziri ya Mambo ya Ndani Yuriy Lubkovych, ambao walikuwa ndani ya ndege hiyo pamoja na watu wengine sita, amesema mkuu wa polisi ya Ukraine katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

"Wenzangu, marafiki zangu. hasara iliyoje. Rambirambi za dhati kwa familia zao," amejibu kwenye Twitter Anton Gerachtchenko, mshauri wa Bw. Monastyrsky.

Mwanasheria huyu wa kitaalamu alikuwa afisini tangu Julai 2021. Mnamo 2019, alikua mwanachama wa Rada, Bunge la Ukraine, chini ya lebo "Mtumishi wa watu", chama cha urais.

Ajali hiyo ilitokea huko Brovary, mji wenye wakazi 100,000 ambao unagusa vitongoji vya mashariki mwa Kyiv. Mapigano makubwa yamekuwa yakihusisha Ukraine na Urusi wakati wanajeshi kutoka Moscow walipojaribu kulazimisha kufungwa kwa mji mkuu katika wiki za kwanza za uvamizi wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.