Pata taarifa kuu
URUSI- UKRAINE- MAPIGANO

Makabiliano makali yameripotiwa kati ya jeshi la Ukraine na Urusi

Mapigano makali yameripotiwa kati ya jeshi la Ukraine na Urusi, katika mji wa Dnipro, mauaji ya raia yakiripotiwa.

Shambulio la Urusi katika mji wa Dnipro, Ukraine, Jumamosi, Jan. 14, 2023.
Shambulio la Urusi katika mji wa Dnipro, Ukraine, Jumamosi, Jan. 14, 2023. AP - Evgeniy Maloletka
Matangazo ya kibiashara

Ukraine inasema watu 40 wakiwemo watoto wameauawa na wengine zaidi ya 30 hawajulikani waliko, huku ikiishtumu wanajeshi wa Urusi kwa kuwalenga raia baada ya kurusha makombora katika makaazi ya watu.

Mji wa Dnipro, umeshuhudia mashambulio mabaya zaidi, tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mwezi Februari mwaka uliopita, lakini Moscow inakanusha madai ya kuwalenga raia wa kawaida.

Aidha, jeshi la Urusi limeendeleza mashambulio katika miji 25 karibu na miji mikubwa ya Bakhmut na Avdiika, ikiwa ni katika harakati za kudhibiti kikamilifu jimbo la Donbas.

Wakati hayo yakijiri, Ukraine inayataka mataifa ya Magharibi kuongezea kazi ya kuipa silaha, ili kuendelea kupambana na wanajeshi wa Urusi.

Uingereza tayari imetangaza kuwa, itatuma magari ya kijesji na vifaa vingine, kulisaidia jeshi la Ukraine, wakati huu Ujerumani nayo ikipata shinikizo kutuma silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.