Pata taarifa kuu

Moscow inalinganisha nchi za Magharibi na Hitler

Mkuu wa diplomasia ya Urusi Sergey Lavrov Jumatano amelinganisha hatua za nchi za Magharibi dhidi ya nchi yake na "suluhisho la mwisho" la utawala wa Nazi la kuwaangamiza Wayahudi, matamshi yanayoakisi nadharia zinazoibuliwa kwa kawaida huko Moscow.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov. © Kommersant/SIPA
Matangazo ya kibiashara

"Kama vile Napoleon alivyokusanya karibu Ulaya yote dhidi ya utawala wa Urusi, kama vile Hitler alivyokusanya na kushinda nchi nyingi za Ulaya ili kuzizindua dhidi ya Umoja wa Kisovieti, leo Marekani imekusanya muungano" dhidi ya Moscow, amesema Bw. Lavrov, wakati wa mkutano na waandishi wa habari mwanzoni mwa mwaka.

Kazi yao ni "ni ile ile: 'suluhisho la mwisho' kwa swali la Urusi. Kama vile Hitler alitaka kutatua swali la Kiyahudi, sasa viongozi wa nchi za Magharibi (...) wanasema bila ubishi kwamba Urusi lazima ishindwe kwa kimkakati," ameongeza.

Iwapo Moscow inazishutumu mara kwa mara nchi za Magharibi kwa kutaka "kuiangamiza" Urusi kwa kuipa Ukraine silaha, matamshi mapya ya Bw. Lavrov huenda yakaibua hisia kali. Mwaka jana, Bwana Lavrov alizua kilio kwa kudai kuwa Adolf Hitler alikuwa na "damu ya Kiyahudi", na kumlazimisha Vladimir Putin kuomba msamaha kwa Waziri Mkuu wa Israeli.

Mkuu wa diplomasia ya Urusi pia alisisitiza tena Jumatano kwamba Moscow iko tayari kusoma "pendekezo lolote zito" la mazungumzo kutoka nchi za Magharibi kusuluhisha mzozo wa Ukraine. "Hatujaona pendekezo zito bado, lakini tutakuwa tayari kuzisoma na kufanya maamuzi," ameongeza, huku akiondoa mazungumzo yoyote na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

"Tunasikia maneno katika miji mikuu ya Magharibi kwamba 'huwezi kuzungumza juu ya Ukraine bila Ukraine'... Lakini ni nchi za Magharibi ambazo zinaamua bila shaka," amesema.

Bw Lavrov pia amedai tena kuondolewa kwa "miundombinu yote ya kijeshi" iliyoko Ukraine na katika nchi jirani na kutishia, kulingana na yeye, "moja kwa moja" Moscow, pamoja na mwisho wa madai ya "ubaguzi" dhidi ya wazungumzaji wa Kirusi nchini Ukraine.

Mzozo huo ulipozua mgogoro kati ya Moscow na nchi za Magharibi, Lavrov amesifu uhusiano wa "kuaminiana" kati ya Urusi na China, "kulingana na uwiano wa maslahi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.