Washirika wa NATO kuipatia Ukraine silaha 'nzito na za kisasa zaidi'
Washirika wa NATO wataipatia Ukraine silaha 'nzito na za kisasa zaidi' ili kuisaidia kukabiliana na mashambulizi ya Urusi, Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg ametangaza siku ya Jumatano.
Imechapishwa:
"Tutakutana (Ijumaa) huko Ramstein (Ujerumani) katika kikundi cha mawasiliano cha Ukraine kinachoongozwa na marekani na ujumbe mkuu itakuwa kuongezwa msaada kwa silaha nzito na za kisasa zaidi," amesema, akiwa nchini Uswisi.
wakati huo huo watu watatu wakuu katika wizara ya mambo ya ndani ya Ukraine wameuawa katika ajali ya helikopta kando ya kitalu katika kitongoji cha mashariki mwa mji mkuu Kyiv.
Waziri wa Mambo ya Ndani Denys Monastyrsky, 42, alikufa pamoja na naibu wake wa kwanza wa waziri na katibu wa serikali.
Watu 16 walikufa wakati helikopta hiyo ilipoanguka huko Brovary, wakiwemo watoto watatu, kulingana na maelezo yaliyosasishwa kutoka kwa rais wa Ukraine.