Pata taarifa kuu

Vita vya Ukraine: Takriban watu 6 wauawa na kadhaa kujeruhiwa Kryvyi Rig, mji wa Zelensky

Urusi imeongeza mashambulizi nchini Ukraine baada ya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani yaliyolenga mji mkuu wa Urusi, Moscow. Shambulio la siku ya Jumatatu liliua takriban watu sita katika mji wa Kryvyi Rig, alikozaliwa Volodymyr Zelensky.

jengo lililoharibiwa katika eneo la biashara la mji wa Moscow baada ya kuripotiwa shambulio la ndege zisizo na rubani huko Moscow, Urusi, mapema Jumapili, Julai 30, 2023.
jengo lililoharibiwa katika eneo la biashara la mji wa Moscow baada ya kuripotiwa shambulio la ndege zisizo na rubani huko Moscow, Urusi, mapema Jumapili, Julai 30, 2023. AP
Matangazo ya kibiashara

Shambulizi la anga la Urusi liliharibu jengo la ghorofa nchini Ukraine siku ya Jumatatu na kuua watu sita na wengine kadhaa kujeruhiwa, huku Urusi ikiongeza mashambulizi yake kufuatia mashambulizi ya ndege zisizo na rubani mjini Moscow.

Mapema asubuhi, eneo la Kryvyi Rig, alikozaliwa Rais wa Ukrain Volodymyr Zelensky, lililoko katikati mwa nchi, lililengwa kwa makombora mawili ya Urusi.

Moja ya makombora hayo liliharibu sehemu nzima ya jengo, na kuua watu sita, ikiwa ni pamoja na msichana wa miaka 10 na mama yake, na kujeruhi 75, kulingana na ripoti iliyosasishwa kutoka kwa mkuu wa utawala wa kijeshi wa jiji hili, Oleksandr Vilkoul.

Wengi wa waliojeruhiwa wanatibiwa nyumbani, lakini karibu wengine ishirini "wanasalia hospitalini", wawili kati yao "wako katika hali vibaya", amesema. Kombora lingine lilipiga jengo la taasisi ya elimu.

"Mashambulizi haya yalipiga majengo ya makazi, jengo la chuo kikuu, maeneo yenye watu wengi. Kwa bahati mbaya, kuna watu waliofariki na wengine kujeruhiwa," Rais Zelensky ameshutumu kwenye Facebook, akilaani"ugaidi wa Urusi".

Katikati ya mwezi Juni,mji wa  Kryvyï Rig ulilengwa na mashambulizi ya anga ya Urusi ambayo yalisababisha vifo vya watu 12. Jengo la ghorofa na ghala, miongoni mwa mambo mengine, viliathirika.

Kusini, huko Kherson, mzee wa miaka 65 aliuawa wakati gari lake liliposhambuliwa na wanajeshi wa Urusi, mamlaka katika eneo hilo imesema.

Urusi, ambayo haikubali kamwe kusababisha vifo vya raia, imekiri kwa upande mwingine kuzidisha mashambulizi ya mabomu nchini Ukraine, huku ikijaribu kutea hatua zake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.