Ukraine: Urusi yafanya mashambulizi kwenye bandari ya mkoa wa Odessa
Ndege kadhaa zisizo na rubani za Urusi zimeshambulia mji mkuu wa Ukraine Kyiv usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano, na kusababisha uharibifu wa mali lakini hakuna majeruhi.
Imechapishwa:
Shambulio la ndege zisizo na rubani pia limefanyika usiku kusini mwa mkoa wa Odessa, bandari kuu ya Ukraine kwenye Bahari Nyeusi. Moto unaendelea. Fuata matukio ya hivi punde katika vita vya Ukraine saa baada ya saa.
Shambulio la ndege zisizo na rubani za Urusi limeharibu miundombinu ya bandari na kusababisha moto mkubwa katika jimbo la Odessa kusini mwa Ukraine, gavana wa eneo hilo Oleg Kiper ametangaza Jumanne usiku.
"Kutokana na shambulio hilo, moto ulizuka katika vituo vya bandari na miundombinu ya viwanda katika eneo hilo," Oleg Kiper ameandika kwenye Telegram. Hakuna majeruhi yalioripotiwa hapo awali.