Pata taarifa kuu

Volodymyr Zelensky amfuta kazi balozi wake nchini Uingereza

Vadym Pristaïko, balozi wa Ukraine nchini Uingereza, hivi karibuni amekuwa akimkosoa sana Rais Volodymyr Zelensky.

Volodymyr Zelensky amejibu wakati wa mkutano na waandishi wa habari, akisema "natambua" msaada mkubwa kutoka raia wa Uingereza.
Volodymyr Zelensky amejibu wakati wa mkutano na waandishi wa habari, akisema "natambua" msaada mkubwa kutoka raia wa Uingereza. © Sergei CHUZAVKOV / AFP
Matangazo ya kibiashara

Volodymyr Zelensky mnamo Ijumaa Julai 21 amemfuta kazi balozi wake nchini Uingereza, Vadym Pristaïko, mtu muhimu katika uhusiano kati ya Kyiv na London. Uamuzi wake ulirasimishwa na amri, iliyochapishwa kwenye tovuti ya ofisi ya rais wa Ukraie. Hakuna sababu iliyotolewa. Lakini inaonekana kama adhabu. Hivi karibuni balozi huyo alikuwa akimkosoa rais wa Ukraine, akijutia "kejeli" yake iliyomlenga Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Ben Wallace, ambaye aliomba kuwepo na umakini zaidi kwa msaada wa kijeshi unaotolewa na washirika wa Kiev.

Mnamo Julai 12, kando ya mkutano wa kilele wa NATO huko Vilnius, Lithuania, Ben Wallace alidai kuwa Uingereza "si Amazon" ya kusambaza silaha kwa Ukraine, akipendekeza kwamba Kiev inaweza kuonyesha "shukrani" zaidi.

Volodymyr Zelensky afurahia msaada wa Uingereza

Uingereza imekuwa mmoja wa wafuasi wenye nguvu wa Kyiv na mmoja wa wafadhili wake wakuu wa silaha tangu kuanza kwa mzozo na Urusi. Volodymyr Zelensky amejibu wakati wa mkutano na waandishi wa habari, akisema "natambua" msaada mkubwa kutoka raia wa Uingereza. "Niambie jinsi nyingine ningeweza kutoa shukrani yangu?" Au tungenaweza kuamka asubuhi, na kutoa maneno yetu ya shukrani kibinafsi kwa waziri mwenyewe? " amesema rais wa Ukraine.

Siku iliyofuata, Vadym Pristaïko alisikitika katika mahojiano na idhaa ya Uingereza ya Sky News kwamba Volodymyr Zelensky alijibu kwa "kejeli kidogo". "Sidhani kuwa kejeli ni nzuri. Hatupaswi kuwaonyesha Warusi kwamba kuna kitu kinaendelea kati yetu, lazima wajue kwamba tunafanya kazi pamoja, "aliongeza, akisisitiza haja ya kutuliza uhusiano na Uingereza. "Ikitokea kitu, Ben anaweza kunipigia simu na kuniambia chochote anachotaka," alisema. Vadym Pristaïko alikuwa balozi wa Ukraine nchini Uingereza tangu Julai 2020. Hapo awali alikuwa waziri wa mambo ya nje kuanzia 2019 hadi 2020.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.