Pata taarifa kuu

Ukraine: Rishi Sunak afanya ziara ya kushtukiza Ukraine na 'kuthibitisha kuiunga mkono'

Kwa mara ya kwanza tangu aingie madarakani, Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amefanya ziara ya kiserikali mjini Kyiv Jumamosi tarehe 19 Novemba. Alichukua fursa hiyo kukutana na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, na kumthibitishia uungaji mkono wa Uingereza kwa Ukraine.

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak akutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, Novemba 19, 2022 mjini Kyiv, Ukraine.
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak akutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, Novemba 19, 2022 mjini Kyiv, Ukraine. AFP - STR
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, ndiye ambaye ametangaza ziara ya kushtukiza ya mwenzake wa Uingereza, Rishi Sunak huko Kyiv. Ni ziara yake ya kwanza tangu kuchukua wadhifa wa kiongozi wa Uingereza.

"Tangu siku za kwanza za vita, Ukraine na Uingereza zimekuwa washirika wa nguvu," Volodymyr Zelensky ameandika kwenye Telegram, akiweka video ya mkutano wake na Rishi Sunak mjini Kyiv.

"Niko hapa leo kusema kwamba Uingereza itaendelea kukuunga mkono," Rishi Sunak amemwambia Rais Zelensky katika video iliyotolewa na ofisi ya rais wa Ukraine. "Tutashirikiana nanyi hadi Ukraine itakapopata amani na usalama inayohitaji na inayostahili."

"Ni somo kubwa la unyenyekevu kuwa nanyi katika nchi yenu leo," amesema pia. "Ujasiri wa raia wa Kiukreni ni msukumo kwa ulimwengu."

Tutawaambia wajukuu wetu historia yenu, jinsi watu wenye ujasiri na wakuu wamesimama dhidi ya shambulio baya, jinsi ulivyopigana, jinsi ulivyojitolea, jinsi ulivyoshinda.

Katika London, Downing Street imesema kuwa Rishi Sunak amesafiri kwenda Kyiv "kuthibitisha uungaji mkono wa Uingereza" kwa Ukraine. "Waziri Mkuu yuko Ukraine leo katika ziara yake ya kwanza huko Kyiv kukutana na Rais (Volodymyr) Zelensky na kuthibitisha uungaji mkono wa Uingereza unaoendelea," Downing Street imesema.

Uingereza "inajua maana ya kupigania uhuru," Rishi Sunak pia ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter. "Tupo pamoja nawe siku zote".

Katika hafla ya ziara hii ya kushtukiza, Rishi Sunak ameahidi jukumu kuipa Ukraine pauni milioni 50 (euro milioni 57) za zana za kijeshi za dhidi ya mashambulizi ya angani nchini Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.