Pata taarifa kuu

Ukraine: Zaidi ya nyumba milioni saba hazina umeme baada ya mashambulizi

Mji mkuu, Kyiv, na miji mingine ya Ukraine, kama vile Lviv au Kharkiv, imekumbwa na masambulizi mapya ya Urusi Jumanne, Novemba 15. Inadaiwa kuwa mtu mmoja ameuawa huko kyiv kufikia sasa. Miundombinu ya nishati imelengwa na mashambulizi hayo. Mamlaka ya mkoa wa Urusi wa Belgorod, unaopakana na Ukraine, pia imetangaza vifo viwili katika masambulizi ya Ukraine kwenye eneo lao.

Lviv, magharibi mwa Ukraine, baada ya mashambulizi ya Urusi mnamo Jumanne, Novemba 15, 2022.
Lviv, magharibi mwa Ukraine, baada ya mashambulizi ya Urusi mnamo Jumanne, Novemba 15, 2022. AFP - YURIY DYACHYSHYN
Matangazo ya kibiashara

Urusi imerusha makumi ya makombora huko Ukraine siku ya Jumanne, Novemba 15. Makombora haya "yalirushwa (...) kutoka Bahari ya Caspian, eneo la (Urusi) la Rostov", na pia "kutoka Bahari Nyeusi", amebaini Yuri Ignat, msemaji wa jeshi la anga la Ukraine.

Moja kwa moja kwenye televisheni ya Ukraine, pia alifafanua kwamba "katika hatua hii, matumizi ya ndege zisizo na rubani hayajaripotiwa" leo.

Ving'ora vya tahadhari ya ulinzi wa anga vimesikika nchi nzima muda mfupi kabla ya saa 9:30 alaasiri saa za Ukraine. Dakika chache baadaye, milipuko ilisikika huko Kyiv, Lviv, magharibi mwa nchi, na Kharkiv, kaskazini-mashariki.

Meya wa mji wa kyiv Vitali Klitschko amehesabu angalau makombora matatu ya Urusi ambayo yalipiga majengo ya makazi katika mji mkuu. "Shughuli za uokoaji na utafutaji zinaendelea," Klitschko ameongeza.

Afisa wa utawala wa rais wa Ukraine ametoa video inayoonyesha jengo la ghorofa tano likiwa linawaka moto.

Na magharibi mwa nchi, "milipuko imesikika huko Lviv. Kila mtu akimbilie eneo salama! ", Amehimiza kwenye Telegraph mwenzake wa mji wa Lviv, Andriy Sadovy, ambaye alifafanua kuwa "sehemu ya jiji (haina) na umeme".

Katika mji wa Rivné, pia magharibi, meya wa mji huo Oleksandre Tretyak aliripoti kwenye mitandao ya kijamii "mashambulizi katika eneo muhimu", bila kutoa maelezo zaidi. "Jiji kwa kiasi fulani halina umeme," amelalamika.

Hali hii inaripotiwa katika jiji la Kremenchuk, katikati mwa Ukraine, ambapo manispaa ya jiji imesikitishwa na "shambulizi dhidi ya miundombinu muhimu karibu na (mji)".

Mji wa Khmelnytskyi, katikati mwa nchi, pia umekumbwa na "mashambulizi mawili", ametangaza gavana wa mkoa, Serguï Gamaliï.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.