Pata taarifa kuu

Jeshi la Ukraine latangaza kuingia Kherson

Jeshi la Ukraine limeingia Kherson, mji muhimu kusini mwa nchi, siku ya Ijumaa (Novemba 11), baada ya kuondoka kwa vikosi vya Urusi, imesema Wizara ya Ulinzi ya Ukraine, shirika la habari la AFP, limeripoti.

Wanajeshi wa Ukraine wakipeleka bunduki kubwa aina ya 2S7 Pion na magari ya kijeshi, wakati mashambulizi ya Urusi dhidi ya Ukraine yakiendelea, karibu na uwanja wa vita katika jimbo la Kherson, Ukraine Novemba 9, 2022.
Wanajeshi wa Ukraine wakipeleka bunduki kubwa aina ya 2S7 Pion na magari ya kijeshi, wakati mashambulizi ya Urusi dhidi ya Ukraine yakiendelea, karibu na uwanja wa vita katika jimbo la Kherson, Ukraine Novemba 9, 2022. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Urusi imesema imemaliza zoezi la kuwaondoa wanajeshi wake katika jimbo la Kherson, Kusini mwa Ukraine. 

Katika taarifa yake ya kila siku, wizara ya ulinzi ya Urusi, imesema vikosi vyote vya Urusi pamoja na vifaa vyao kijeshi vimeondoka magharibi mwa mto Dnipro unaotenganisha jimbo la Kherson na maeneo mengine ya Ukraine. Taarifa hiyo imearifu kuwa vikosi hivyo vimepelekwa ukingo wa mashariki mwa mto huo na kwenye operesheni hiyo Urusi imesema hajaijapoteza askari hata mmoja wala kifaa chochote cha kijeshi.

Hata hivyo, imesisitiza kuwa jimbo hilo ni eneo lake. Mapema hivi leo, ndege za kivita za Urusi, zilishambulia makaazi ya watu katika mji wa Mykolaiv, karibu na Kherson na kusababisha vifo vya watu saba. 

Ukraine inasema inathathmini kwa makini uamuzi huo wa Urusi kuondoa wanajeshi wake, katika jimbo hilo ambalo wamekuwa wakidhibiti tangu mwezi Februari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.