Pata taarifa kuu

Kuondoka kwa askari wa Urusi Kherson ni 'ushindi mkubwa' kwa Ukraine

Jumatano hii, Novemba 9 Moscow ilitangaza kuondoka kwa wanajeshi wa Urusi katika jimbo la Kherson. Tangazo ambalo wengi wanaona kuwa ni kushindwa kwa Urusi. 

Wanajeshi wa Urusi katika jimbo l Kherson, Mei 20, 2022.
Wanajeshi wa Urusi katika jimbo l Kherson, Mei 20, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi wa Urusi walioko Kherson walikuwa ni tishio kwa wakaazi wa miji ya Odessa na Mykolaiv ambao waliokuwa kuwa wakihofia kutokea kwa shambulio, miji miwili ambayo ilikuwa imezingirwa na wanajeshi wa Urusi walioko Kherson upande mmoja na wale waliowekwa Transnistria kwa upande mwingine, eneo lililojitenga la Moldova chini ya ushawishi wa Urusi kwa miaka 30.

Kwa mujibu wa Oleksiy Hontcharenko, mbunge kutoka mji wa Odessa katika Bunge la Ukraine (Rada), tangazo hili ni ushindi kwa Ukraine: "Ni ushindi mkubwa kwa Ukraine kwa sababu ni jiji pekee lililo katikati ya Ukraine, ambalo lilichukuliwa na Urusi wakati wa uvamizi ulioanza Februari 24. Na sasa Urusi itajiondoa kutoka Kherson. "

Kwa mwakilishi huyu aliyechaguliwa, kuondoka kwa wanajeshi wa Urusi katika jimbo hili pia ni muhimu kwa upande wa kimkakati, kwa sababu Kherson ilikuwa ngome ya jeshi la Urusi kuelekea Odessa na kwa upande wa Ukraine, mji ambao uko karibu na Bahari nyeusi. Jimbo la Kherson pia lingetumiwa na vikosi vya Urusi vilivyoko katika mji wa Transnistria, eneo la Moldavia linalokaliwa na Urusi kwa miaka thelathini.

"Ndiyo maana ni muhimu sana, "amekumbusha Oleksiy Hontcharenko. Nadhani baada ya hapo hatuwezi kusema kwamba Ukraine ilishinda vita. Lakini tunaweza kusema kwamba Urusi ilipoteza vita. "

Siku ya Alhamisi, Volodymyr Zelensky alisema kwamba tunapaswa kuwa waangalifu na tangazo hili kutoka Moscow. Je, hili tangazo ni mbinu ya kuwa makini kweli? Oleksiy Hontcharenko anaona kwamba kamandi ya kijeshi ya Ukraine itapanga operesheni hii ya kuikomboa Kherson kwa njia ya kitaalamu sana: “Wao ni wataalamu sana, wazuri sana kwa ujumla. Kwa hivyo sina wasiwasi. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.