Pata taarifa kuu

Ukraine yashuku kuwa Moscow imetega mabomu katika majumba na mitaro Kherson

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatazama kwa makini hatua ya Urusi kutangaza kuwa inaondoa vikosi vyake katika jimbo la Kherson baada ya mapigano ya miezi kadhaa sasa.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky. AP - Genya Savilov
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii ya rais Zelenskyy, inakuja wakati huu Urusi ikithibitisha kuanza kuondoa vikosi vyake katika jimbo hilo, iliyokuwa imeliteka tangu ilipoivamia Ukraine mwezi Februari, baada ya Kamanda wa Urusi nchini Ukraine Jenerali Sergei Surovikin, kusema imekuwa ngumu kuendelea kupambana katika êneo hilo. 

Mshauri wa rais Zelenskyy anasema baada ya Urusi kuondoa katika jimbo hilo, inataka kuhakikisha kuwa, mpango wake ni kuhakikisha kuwa Kherson unakuwa mji wa maafa. 

Katika hatua nyingine, Ukraine inasema wanajeshi wake wamechukua miji na vijiji zaidi ya 10 Kusini mwa jimbo la Kherson, baada ya Urusi kutangaza kuwa inawaondoa wanajeshi wake katia mji huo. 

Naye rais wa Marekani Joe Biden, amesema uamuzi wa Urusi kuondoa wanajeshi wake katika jimbo hilo, unaonesha kuwa, jeshi lake lina changamoto ngumu. 

Katibu Mkuu wa Jeshi la NATO, Jens Stoltenberg naye amesema hatua ya nchi yake, inaonesha kuwa, Urusi inapata shinikizo kutoka kwa Ukraine na anatumai kuwa, hatua hii inaonesha ushindi wa Ukraine. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.