Pata taarifa kuu

Makumi kwa maelfu ya Waitaliano waandamana Jumamosi hii kwa ajili ya amani nchini Ukraine

Makumi ya maelfu ya watu wameandamana mjini Roma siku ya Jumamosi kudai amani nchini Ukraine na kuiomba serikali ya Italia kusitisha kutuma silaha kupigana dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Waziri mkuu mpya wa siasa kali za mrengo wa kulia Giorgia Meloni amesema hilo halitabadilika na serikali inapanga kutuma vifaa vya ziada vya kijeshi hivi karibuni.
Waziri mkuu mpya wa siasa kali za mrengo wa kulia Giorgia Meloni amesema hilo halitabadilika na serikali inapanga kutuma vifaa vya ziada vya kijeshi hivi karibuni. REUTERS - YARA NARDI
Matangazo ya kibiashara

"Hapana kwa vita. Hapana kwa kutuma silaha",  maneno ambayo yameandikwa kwenye bango kubwa lililobebwa na waandamanaji - Waandamanaji walikuwa 30,000, kulingana na takwimu za polisi zilizonukuliwa na vyombo vya habari vya Italia - ambao wameimba: "toweni nafasi kwa amani!".

Italia, moja ya wanachama waanzilishi wa NATO, imeunga mkono Ukraine tangu kuanza kwa mzozo huo mwishoni mwa mwezi wa Februari, hasa kwa kuipatia silaha.

Waziri mkuu mpya wa siasa kali za mrengo wa kulia Giorgia Meloni amesema hilo halitabadilika na serikali inapanga kutuma vifaa vya ziada vya kijeshi hivi karibuni.

Lakini baadhi, ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu wa zamani Giuseppe Conte, wanaamini Italia inapaswa kuongeza mazungumzo badala ya kutuma silaha nchini Ukraine.

"Silaha zilitumwa mwanzoni kwa misingi kwamba ingezuia kuongezeka kwa mashambulizi," mmoja wa waandamanaji, Roberto Zanotto, ameliambia shirika la habari la AFP. "Miezi tisa baadaye, inaonekana kwangu kuwa kumekuwa na ongezeko la mapigano. Angalia ukweli: kutuma silaha hakusaidii kusitisha vita, silaha zinachangia kuchochea vita".

Kulingana na Sara Gianpietro, mwanafunzi, mzozo unaendelea kwa kupeleka silaha nchini Ukraine, jambo ambalo "lina madhara ya kiuchumi kwa nchi yetu, lakini pia kwa heshima ya haki za binadamu".

Siku ya Ijumaa, mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa ya G7, ikiwemo Italia, waliahidi kuendelea kuiunga mkono Ukraine katika mapambano yake dhidi ya Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.