Pata taarifa kuu

Urusi: Maandamano na malalamiko kutoka kwa wapiganaji walioajiriwa vyaongezeka

Wanajeshi wa Urusi waliohamasishwa waliandamana usiku wa Ijumaa Novemba 4 kuamkia Jumamosi, katika kambi zao karibu na jiji la Kazan. Wanapinga mazingira mabaya ya maisha yao: ukosefu wa maji, chakula na kuni. Matukio ya aina hii yamekuwa yakiongezeka kote nchini Urusi katika siku za hivi karibuni.

Bango la propaganda la jeshi la Urusi katika kampeni ya kuajiri wanajeshi wapya katika mitaa ya Moscow.
Bango la propaganda la jeshi la Urusi katika kampeni ya kuajiri wanajeshi wapya katika mitaa ya Moscow. AFP - YURI KADOBNOV
Matangazo ya kibiashara

Video zilisambazwa kwa mara ya kwanza kwenye mitandao ya kijamii ya Urusi kabla ya kuthibitishwa na kuchukuliwa kwenye vyombo vya habari. katika video hizi kunaonekana umati wa watu, katikati ya usiku, nje, katika kile kinachoonekana kuwa kambi ya kijeshi. Makumi ya watu waliovalia sare zisizolingana wakimzunguka afisa wa Urusi. Wanamlemea kwa lawama na matusi, wanalalamika kwa kupokea tu bunduki zenye kutu za miaka ya 1970, huku wakikosa maji, hawapewi chakula, au hata kuni za kupasha joto. Wanajeshi hao wanadai kupata, angalau, kitu cha kuweza kujiosha na kusafisha nguo zao.

Malalamiko ya pande zote

Ni tukio la dalili la kufunuliwa kwa uhamasishaji nchini Urusi. Baada ya mkanganyiko kwa wiki za kwanza na hofu ya wale waliohamasishwa, matatizo yanaendelea katika kambi. Ukosefu wa vifaa, mabweni, na wakati mwingine hata chakula na maji katika kambi ambayo wakati mwingine sio safi au chakavu. Hakuna kitu kilicho tayari kwa kuwapokea wapiganaji wapya wanaoajiriwa. Malalamiko yanaibuka kutoka kote nchini, yakirekodiwa na waajiri wenyewe kwenye simu zao za rununu. Na yanasambazwa sana na watu wanaopinga vita.

Baadhi ya hali hushughulikiwa kwa msingi wa kesi kwa kesi na mamlaka. Lakini hata hivyo, majibu haya ya mara moja hayatoshi kuficha mapungufu makubwa ya vifaa vya jeshi la Urusi katika kusimamia na kutoa mafunzo kwa wanajeshi hawa wapya, hata kabla ya swali lolote la kuwapeleka kwenye uwanja wa mapigano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.