Pata taarifa kuu

Rais wa Ukraine ayaita mashambulizi ya Urusi kama ya kigaidi, Moscow yateka maeneo kadhaa

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ameishutulu Urusi kwa kuamua kuvamia vituo vyake vya nishati, tukio ambalo amelifafanisha kama la kigaidi. 

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema hatua ya Urusi kushambulia miundo mbinu yake ya nishati, imewaacha watu zaidi ya Milioni 4.5 bila umeme nchini humo.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema hatua ya Urusi kushambulia miundo mbinu yake ya nishati, imewaacha watu zaidi ya Milioni 4.5 bila umeme nchini humo. AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii ya rais Zelensky imekuja wakati huu wanajeshi wa Urusi wakiripotiwa, kuchukua maeneo kadhaa yaliyokuwa yanadhibitiwa na wanajeshi wa Ukraine. 

Kiongozi huyo wa Ukraine amesema hatua ya Urusi kushambulia miundo mbinu yake ya nishati, imewaacha watu zaidi ya Milioni 4.5 bila umeme nchini humo. 

Ripoti zaidi zinasema, wanajeshi wa Urusi huenda wakajiandoa katika mji wa Kherson ulio Kusini mwa nchi hiyo baada ya kuonekana kulemewa na wanajeshi wa Ukraine. 

Awali, Urusi ilinukuliwa ikisema wanajeshi wake hawana mpango wa kuondoka katika mji huo, lakini picha zinazoonekana kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha kuwa, mji huo hauna bendera za Urusi kama ilivyokuwa hapo awali. 

Tangu mwezi Oktoba, jeshi la Ukraine, limeonekena likisonga mbele katika mji huo na kuchukua maeneo ya kimakati kama madaraja na kuwafanya wanajeshi wa Urusi kurudi nyuma. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.