Pata taarifa kuu

Shambulio la ndege isiyo na rubani Crimea: Moscow yajiondoa kwenye makubaliano ya nafaka

Kulingana na jeshi la Urusi, shambulio la ndege isiyo na rubani ilizuiliwa na meli zake huko Sevastopol Bay, Crimea. Urusi inalaumu “serikali ya Kyiv” na “wataalamu wa Uingereza” kwa shambulizi hilo. 

Wanajeshi wa Jeshi la Wanamaji la Urusi wakijiandaa kwa mazoezi ya kupiga mbizi mbele ya meli iitwayo Tarantul-III iliyowekwa kwenye ghuba ya bandari ya Crimea ya Sevastopol mnamo 2014.
Wanajeshi wa Jeshi la Wanamaji la Urusi wakijiandaa kwa mazoezi ya kupiga mbizi mbele ya meli iitwayo Tarantul-III iliyowekwa kwenye ghuba ya bandari ya Crimea ya Sevastopol mnamo 2014. AFP - OLGA MALTSEVA
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Urusi linahusisha Ukraine lakini pia Uingereza shambulizi hili la ndege zisizo, katikati ya tahadhari zote za Urusi Jumamosi hii, kwani London pia inashutumiwa na Moscow kwa kuhusika katika suala la mabomba ya Nord Stream. Shirikisho la Urusi linatangaza hatua katika Umoja wa Mataifa, na kujiondoa katika makubaliano kuhusu nafaka.

Mamlaka zinazoiunga mkono Urusi katika peninsula ya Crimea, iliyoshikiliwa na Shirikisho la Urusi mwaka 2014, ilitangaza mapema Jumamosi hii Oktoba 29 kwamba meli za meli za Urusi katika Bahari Nyeusi zimezuia shambulio lililofanywa kwa kutumia drones katika Ghuba ya Sevastopol. Vyombo vyote vya kushambulia vilipigwa risasi, waliongeza.

Mapema leo Jumamosi, wizara ya ulinzi ya Urusi ilidai kikosi cha wataalamu wa jeshi la Uingereza kilichofanikisha mpango wa shambulizi la siku Jumamosi dhidi ya meli za Urusi kwenye rasi ya Crimea - ambayo Moscow iliinyakua kutoka Ukraine mnamo mwaka 2014- ndiyo kilitumika kufanya "shambulizi la kigaidi" kwenye mabomba ya Nord Stream 1 na 2 Septemba 26.

Jeshi la Urusi liliituhumu Ukraine kufanya shambulizi kubwa la ndege isiyo na rubani dhidi ya kamanda yake ya majini katika eneo la Bahari Nyeusi na kwenda mbali zaidi ikidai Uingereza iilisaidia Kyiv kufanikisha hujuma hiyo.

Moscow inasitisha ushiriki katika mpango wa mauzo ya nafaka kutoka Ukraine

Makubaliano kati ya Urusi na Ukraine juu ya usafirishaji wa nafaka kutoka bandari ya Ukraine yalitiwa saini mwishoni mwa Julai.

Mazungumzo hayo yalihitimishwa kwa upatanishi wa Uturuki na Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.