Pata taarifa kuu

Ukraine: Volodymyr Zelensky azuru Kherson iliyokuwa ikikaliwa na Urusi

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky leo Jumatatu ametembelea Kherson, mji muhimu kusini mwa nchi hiyo uliochukuliwa na jeshi la Ukraine kutoka mikononi mwa vikosi vya Urusi wiki iliyopita, chanzo kutoka ofisi ya rais wa Ukraine kimeliambia shirika la habari la AFP.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky atembelea jiji la Kherson, Novemba 14, 2022.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky atembelea jiji la Kherson, Novemba 14, 2022. © AP
Matangazo ya kibiashara

Volodymyr Zelensky amezuru mji huo, huku akivalia mtindo wa kijeshi, akiwa amezungukwa na walinzi wenye silaha nzito, lakini bila kuvaa kofia ya chuma au vazi la kujilinda, kulingana na video zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa upande wake, Kremlin imesisitiza Jumatatu kwamba mji wa Ukraine wa Kherson ni wa Urusi, ikijibu Rais Volodymyr Zelensky kuwasili katika mji huo. 

Vikosi vya Urusi vilijiondoa katika Kherson mnamo Novemba 9. Na hii ni baada ya tangazo lililotolewa na Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu. Wanajeshi wa Urusi waliondoka mjini humo baada ya kuushikilia kwa miezi minane, na kuacha uwanja wazi kwa wanajeshi wa Ukraine kuingia mjini humo siku ya Ijumaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.