Pata taarifa kuu

Mlipuko nchini Poland: Moscow yakanusha kuhusika na shambulio lililoua watu wawili

Moscow imekanusha mara moja kuhusika na mlipuko wa bomu baada ya vifo vya watu wawili mashariki mwa Poland Jumanne jioni Novemba 15. Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema hivi baadaye: "Taarifa za vyombo vya habari na wanasiasa kuhusu kudondoka kwa makombora ya Urusi kwenye arhdi ya Poland ni uchochezi wa makusudi kwa madhumuni ya kuongeza vitisho na uhasama dhidi ya Ukraine na majirani zake wanaoiunga mkono". Hata hivyo Kremlin imekaribisha kujizuia kwa Marekani.

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov.
Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Hii ilikuwa kabla ya taarifa za Joe Biden bila kujumuisha jukumu la Urusi kwa kile kilichotokea nchini Poland, wakati mvutano ulikuwa bado uko kwenye kilele chake. “Nani ananufaika na tukio hilo? Mtaalamu Komsomolskaya Pravda amejibu asubuhi hii swali ambalo alijiuliza kwa kuorodhesha kwanza Kyiv kisha, nchi za kwanza katika maeneo ya Urusi, Poland na Uingereza. Mwenyekiti wa Baraza la Urusi la Sera ya Mambo ya Nje na Ulinzi, Fyodor Lukyanov, aliyenukuliwa na Gazeti la Kommersant, amebaini kwamba “ni nchi za Ulaya ya Kati na Mashariki ndizo ziko mstari wa mbele hapa. Hali hi inaongeza hatari zaidi. Vituo vinavyoitwa "Z" vinavyounga mkono mzozo huu havikuwataja wawili hao waliouawa nchini Poland lakini vimeongea kwa pamoja kuhusu "kuharibiwa kwa trekta ya Poland kama sababu ya Vita vya dunia vya 3".

Hakuna makabiliano ya wazi kati ya Urusi na Magharibi, lilisema jana usiku Gazeti la mtandaoni la The Bell ambalo linaona kuwa "sio muhimu kujua ni nini kilitokea katika ardhi ya Poland. Kama ilivyo kwa ndege ya Boeing Malaysia iliyoanguka katika jimbo la Donbass mnamo 2014; ni Urusi ambayo itawajibika.” Na gazeti hilo linakumbusha: "janga hili lilisababisha vikwazo vizito zaidi kabla ya 2022", kabla ya kuongeza kuwa "tukio hili hakika litazidisha mzozo".

Wakati NATO bado iko katika mkutano wa dharura mjini Brussels, msemaji wa Wizara ya Ulinzi Igor Konashenkov amesema katika mkutano wake wa kila siku na waandishi wa habari: "Tungependa kusisitiza kwamba mashambulizi yetu ya usahihi wa hali ya juu yamelenga katika ardhi ya Ukraine na katika umbali wa juu zaidi wa kilomita 35 kutoka mpaka wa Ukraine na Poland. 

Rais wa Marekani Joe Biden hapo awali alikuwa amewaarifu wanachama wa G7 na NATO kwamba anaamini mlipuko wa Jumanne nchini Poland ulisababishwa na shambulio la kombora la ulinzi wa anga la Ukraine, ambalo msemaji wa Kremlin alisema: "Hakukuwa na sababu ya kuongezeka kwa uhasama. Mnaelewa kwamba Poland walikuwa na uwezo wao wa kutoa taarifa mara moja kwamba haya yalikuwa mabaki ya kombora la ulinzi wa anga la S 300. Na wataalam wote wanaelewa kuwa haiwezi kuwa kombora la kijeshi la Urusi. "

Hata hivyo Wizara ya mambo ya nje ya Poland imesema kuwa "kombora lililotengenezwa na Urusi" lilitua katika eneo lake na kuua watu wawili katika kijiji cha Przewodow.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Lukasz Jasina aliongeza kuwa balozi wa Urusi nchini Poland ameitwa kutoa "maelezo ya kina mara moja" juu ya tukio hilo.Taarifa hiyo haisemi ni nani aliyerusha kombora hilo na pande zote mbili katika mzozo huo zimetumia mabomu yaliyotengenezwa na Urusi.

Przewodow iko kwenye mpaka wa Poland na Ukraine, na kaskazini mwa jiji la Lviv.Makombora yaripotiwa kushambulia kijiji cha Przewodow, yapata maili nne (6.4km) kaskazini mwa Ukraine, mapema Jumanne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.