Pata taarifa kuu
UKRAINE- URUSI -VITA

Ukraine: UN na Msalaba Mwekundu wanapaswa kuchunguza vifo vya wafungwa

Ukraine imetoa wito kwa Umoja wa Mataifa na Shirika la Msalaba Mwekundu kuruhusiwa kuchunguza vifo vya zaidi ya wafungwa 50 wa Kivita wa Ukraine (POWs) katika shambulio dhidi ya maeneo yanayokaliwa kimabavu.

Mabaki ya jengo la jela mjini  Olenivka lililoharibiwa kwa bomu  Julai 29, 2022.
Mabaki ya jengo la jela mjini Olenivka lililoharibiwa kwa bomu Julai 29, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake Shirika la Msalaba Mwekundu limesema kuwa linatafuta mbinu ya kufika katika gereza hilo ili kusaidia katika shughuli ya kuwaondoa na kuwapa matibabu watu waliojeruhiwa wakati wa shambulio hilo.

Nchi za Ukraine na Urusi zimeendelea kushutumiana kuhusu ni nani alitekeleza shambulio katika gereza hilo.

Maafisa wa Urusi wanadai kuwa, wafungwa wengine 75 walijeruhuiwa katika shambulio hilo la roketi, lililolenga gereza la Olenivka.

Hata hivyo, jeshi la Ukraine limekanusha madai ya kutekeleza shambulio hilo na badala yake kulishtumu jeshi la Urusi.

Aidha, Kiev inasema madai ya Moscow yanalenga kuficha ushahidi wa jeshi lake kuendelea kutekeleza visa vya unyanyasaji katika gereza hilo.

Rais Volodymyr Zelensky alielezea tukio hilo kama "uhalifu wa kivita uliopangwa na Urusi."

Katika hatua nyingine, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza, imesema Urusi inatumia maafisa wa usalama wa kampuni binafsi ya Wagner kulinda usalama katika maeneo mbalimbali inayodhibiti, Mashariki mwa Ukraine.

Wakati uo huo, rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema nchi yake iko tayari kuanza tena kusafirisha nafaka kupitia bandari nyeusi na kinachosubiriwa ni idhini kutoka kwa Umoja wa Mataifa na Uturuki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.