Pata taarifa kuu

Ukraine kupewa ndege zaidi za kijeshi katikati mwa ziara ya Volodymyr Zelensky London

Rais wa Ukraine amefanya ziara ya kushtukiza nchini Uingereza Jumatano hii, Februari 8. Hii ni mara ya pili kwa Volodymyr Zelensky kuondoka nchini mwake tangu kuanza kwa vita. Jeshi la Uingereza linazungumzia uwezekano wa kupeleka ndege kwa jeshi la Ukraine.

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak, na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, Februari 8, 2023.
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak, na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, Februari 8, 2023. AFP - JUSTIN TALLIS
Matangazo ya kibiashara

Ziara hiyo imetangazwa saa chache tu mapema, anasema mwandishi wetu wa London, Émeline Vin. Kabla ya mkutano kati ya Volodymyr Zelensky na Rishi Sunak, Downing Street inmebaini kwamba London itaimarisha zaidi mafunzo yanayotolewa na jeshi la Uingereza kwa wanajeshi wa Ukraine. Marubani na Wanamaji kwa hivyo watafunzwa kutumia vifaa vilivyotolewa na NATO - hili ni ombi la muda mrefu kutoka kwa Kyiv. Ahadi hii ni pamoja na wanajeshi 10,000 wa Ukraine ambao tayari wamepata mafunzo katika muda wa miezi sita iliyopita, na 20,000 ambao wanatakiwa kupewa mafunzo mwaka huu. Waziri Mkuu pia anasisitiza ahadi yake ya kuuipa Ukraine vifaru aina ya Challenger 2.

Volodymyr Zelensky amechukua fursa hiyo kwa mara nyingine tena mbele ya wabunge wa Uingereza kuwahimiza washirika wake wa Magharibi kumpatia "silaha muhimu" ili kukomesha uvamizi wa Urusi, ikiwa ni pamoja na ndege za kivita. "Ninawaomba, nyinyi na ulimwengu - maneno rahisi, lakini muhimu sana: ndege za kivita kwa Ukraine, mbawa za uhuru. Rais Zelensky pia alimpa Spika wa Bunge la Uingereza kofia ya rubani wa Ukraine ambaye aliandika: "Tuna uhuru, tupe mbawa za kuulinda". Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amelitaka jeshi la Uingereza kuchunguza uwezekano wa kupeleka ndege kwa jeshi la Ukraine, Downing Street imesema siku ya Jumatano, na kuhakikishia hata hivyo kwamba hii inaweza tu kuwa "suluhisho la muda mrefu".

Adhabu za ziada

Vikwazo vipya dhidi ya Urusi pia vimetangazwa, hasa dhidi ya sekta ya silaha. Vikwazo hivyo vipya vinalenga "kampuni sita zinazosambaza vifaa vya kijeshi kama vile ndege zisizo na rubani kwa ajili ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine", Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza imesema katika taarifa. "Watu wanane na kampuni moja inayohusishwa na mitandao mbovu ya kifedha" karibu na Kremlin pia vinakabiliwa na vikwazo vipya, ambavyo ni pamoja na kuvifungia mali.

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak aliahidi Jumatano kuendelea kuunga mkono Ukraine ili kuruhusu ushindi wa "maamuzi [...] mwaka huu", muda mfupi baada ya kuwasili London kwa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky. Rais wa Ukraine ameishukuru Uingereza, "moja ya nchi za kwanza" kuisaidia Ukraine kijeshi na kifedha. Uingereza ni mfadhili mkubwa wa pili wa kifedha wa Ukraine baada ya Marekani tangu kuanza kwa mzozo huo. Ziara hiyo - na mazungumzo kati ya wawili hao- inapaswa kuwezesha London kuthibitisha uungaji mkono wa Uingereza kwa mipango ya Ukraine "kufanya kazi kwa amani ya muda mrefu na ya kudumu".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.