Pata taarifa kuu

Zaidi ya mali na makampuni 500 ya Ukraine yaliyoko Crimea kutaifishwa

Wabunge wa Bunge la Crimea walmekubali - kwa kauli moja - kutaifisha zaidi ya mali na makampuni 500 ya Ukraine yalioko katika eneo hili lililounganishwa tangu 2014. Sehemu ya fedha zitakazokusanywa zitatumika kufadhili operesheni ya kijeshi ya Urusi nchini Ukraine.

Wanajeshi wa Urusi waandamana Sevastopol huko Crimea mnamo Mei 5, 2022.
Wanajeshi wa Urusi waandamana Sevastopol huko Crimea mnamo Mei 5, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

Mali ya benki, viwanda na mali ya viongozi wakuu wakuu wa Ukraine na wale wanaowaunga mkono kwenye eneo hilo zimetaifishwa. Kwa hivyo bunge la eneo hilo linaruhusu serikali ya Urusi kupata mapato mapya ya kifedha, ambayo sehemu yake inasemekana kutumika kufadhili operesheni ya jeshi la Urusi nchini Ukraine.

Ingawa fedha zilizopatikana hazijafichuliwa, mashirika ya Urusi yanaripoti kwamba mali za Rinat Akhmetov, tajiri zaidi nchini Ukraine, na vile vile za bilionea Igor Kolomoiski, benki kadhaa za Ukraine, viwanda kadhaa na zile za kilabu cha soka cha Dynamo Kyiv zinalengwa na hatua hii.

Jibu kwa kuzuiwa kwa mali za Urusi katika nchi za magharibi

Mwishoni mwa mwezi Oktoba 2022, Sergei Aksyonov, mkuu wa Jamhuri ya Crimea, alikuwa tayari ametangaza kutaifisha makampuni makubwa kwenye peninsula ambayo viongozi wake wanaunga mkono serikali ya Kyiv. Msururu wa hatua zinazopaswa kujibu kuzuiwa kwa mali ya Benki Kuu ya Urusi katika nchi za magharibi, pamoja na kuzuiwa kwa mali za viongozi wengi wa Urusi katika nchi kadhaa za Ulaya, Uingereza au Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.