Pata taarifa kuu
UCHUMI-DIPLOMASIA

Kwa kukwepa vikwazo, Moscow yataka kufungua benki inayodhibitiwa na Urusi nchini India

Hili ni pendekezo kali ambalo Moscow inatoa kwa New Delhi ili kukwepa vikwazo vilivyowekwa kwa mfumo wa benki wa Urusi. Tangu kuanza kwa vita nchini Ukraine, India imetaka kuwezesha miamala ya rupia-ruble, lakini Benki Kuu ya Urusi inataka kwenda haraka.

Makao makuu ya Benki Kuu ya Shirikisho la Urusi huko Moscow.
Makao makuu ya Benki Kuu ya Shirikisho la Urusi huko Moscow. AFP - NATALIA KOLESNIKOVA
Matangazo ya kibiashara

Kadiri mzozo unavyozidi kuzorota, ndivyo India, mnunuzi mkuu wa silaha na mafuta, inavyozidi kuwa mshirika muhimu wa kibiashara wa Urusi. Shida ni kwamba biashara inatatizwa na kutengwa kwa Urusi kutoka kwa mfumo wa uhamishaji pesa wa kimataifa wa Swift.

Gazeti la Indian Express linafichua Jumamosi hii kwamba Gavana wa Benki ya Urusi, Vladimir Chistyukhin, amejitolea kufungua moja kwa moja benki inayodhibitiwa na Urusi kwenye ardhi ya India. Hii itaruhusu taasisi za kifedha za India kutumia moja kwa moja mfumo wa muamala wa Benki ya Urusi wa SPFS.

'Hakuna maendeleo yaliyotolewa'

Waziri wa mambo ya nje wa India hivi majuzi aliahidi kusambaza vipuri vya ndege na treni za Urusi. Lakini Urusi inaonyesha kutoridhika na maelewano ya kifedha na India, ambayo inachukulia kuwa polepole sana. "Hakuna maendeleo ambayo yamefanywa," Vladimir Chistyukhin amesema.

Hata hivyo India ilifungua akaunti tisa zinazoitwa "Vostro" mnamo mwezi Novemba. Benki za Urusi zinaweza kuzitumia kutoa ankara moja kwa moja kwa rupia bila kupitia dola. Miongoni mwa hizo ni benki ya kampuni kubwa ya Urusi ya GazProm, Moscow ikiwa muuzaji wa kwanza wa mafuta nchini India.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.