Pata taarifa kuu

NATO yatoa wito kwa Moscow kuheshimu mkataba wa nyuklia wa New Start

Jumuiya ya Kujihami ya nchi za Magharibi, NATO, imeonyesha 'wasiwasi' wake Ijumaa hii, Februari 3, kuona Moscow 'inashindwa katika majukumu yake' kutokana na mkataba wa New Start, ikitoa wito kwa Urusi kuheshimu makubaliano ya hivi karibuni ya kutokomeza silaha za nyuklia yanayohusisha na Marekani.

Picha ya skrini iliyochukuliwa kutoka kwa video iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Urusi mnamo Aprili 20, 2022 ambayo inaonyesha kombora la masafa marefu la Sarmat likirushwa katika eneo la majaribio la Plesetsk, Urusi.
Picha ya skrini iliyochukuliwa kutoka kwa video iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Urusi mnamo Aprili 20, 2022 ambayo inaonyesha kombora la masafa marefu la Sarmat likirushwa katika eneo la majaribio la Plesetsk, Urusi. AFP - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

"Tunatoa wito kwa Urusi kutimiza majukumu yake chini ya Mkataba wa New Start kwa kuwezesha ukaguzi uliopangwa kwenye eneo lake na kuanza tena ushiriki wake katika Tume ya Ushauri ya Nchi Mbili, chombo cha utekelezaji wa mkataba," imesema, Ijumaa hii, Februari 3, taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Muungano wa Atlantiki. Kwa upande wake, Urusi ilishutumu Marekani mnamo Februari 2 kwa "kuharibu mfumo wa kisheria" wa New Start.

Mahusiano yazorota

Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu za nyuklia uko chini kabisa tangu kuanza kwa mashambulizi ya kijeshi ya Urusi nchini Ukraine, huku Washington ikiiunga mkono Kyiv kwa msaada wa kifedha na kijeshi. Rais wa Urusi Vladimir Putin ameibua kitisho cha matumizi ya silaha za atomiki katika mzozo wa Ukraine, na kuzua tena hofu ya mzozo wa nyuklia.

"Washirika wanatambua kwamba mkataba mpya wa Start unachangia utulivu wa kimataifa kwa kupunguza nguvu za kimkakati za nyuklia za Urusi na Marekani", inasisitiza NATO. "Kwa hiyo ni kwa wasiwasi huo kwamba tunaona kwamba Urusi inashindwa kutimiza majukumu ya kisheria yaliyowekwa juu yake" na mkataba huo, Muungano wa Atlantiki umebaini. Moscow ilikuwa imetangaza kwa ufanisi - mwanzoni mwa mwezi Agosti 2022 - kusimamisha ukaguzi wa Marekani uliopangwa kwenye maeneo yake ya kijeshi ndani ya mfumo wa mkataba wa New Start, kuhakikisha kuchukua hatua kwa kukabiliana na vikwazo vya Marekani kwa ukaguzi sawa wa Kirusi nchini Marekani.

Kisha Moscow iliahirisha kwa muda usiojulikana kikao cha tume ya ushauri ya nchi mbili juu ya mkataba huo, ambacho kilikuwa kifanyike huko Cairo kuanzia Novemba 29 hadi Desemba 6, ikishutumu Washington kwa "uadui" na "uhasama". Mkataba huo ulitiwa saini na rais wa Marekani Barack Obama mwaka wa 2010, mkataba wa New Start unaweka mipaka ya silaha za nchi hizo mbili hadi kufikia upeo wa vichwa 1,550 vilivyotumwa kwa kila upande, punguzo la karibu 30% kutoka kwa kikomo kilichowekwa hapo mwaka 2002. Pia unnaweka idadi ya ndege 800.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.