Pata taarifa kuu

Viongozi wa EU wajadili kuimarisha vikwazo zaidi dhidi ya Urusi

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wapo jijini Kyiv kwa ajili ya mazungmzo na uongozi wa Ukraine, wakati huu wakiahidi vikwazo zaidi dhidi ya Urusi. 

Mkutano kati ya Tume ya Ulaya na serikali ya Ukraine huko Kyiv, Februari 2, 2023.
Mkutano kati ya Tume ya Ulaya na serikali ya Ukraine huko Kyiv, Februari 2, 2023. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Tume hiyo Ursula von der Leyen, aliwasili jana jijini Kyiv kwa treni kwa maandalizi ya kikao cha leo kuonesha uungwaji mkono kwa Ukraine. 

Mkutano huu unafanyika kuelekea tarehe 24, mwaka mmoja tangu Urusi ilipoivamia Ukraine, ambayo imekuwa ikitaka kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya, lakini inavyoonekana ndoto hiyo haitatimia hivi karibuni. 

Katika mkutano huo, viongozi wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kumhakikishia rais Volodomyr Zelensky kuendelea kusimama naye, kwa kuipa nchi yake misaada ya kifedha na msaada wa kjeshi ili kuishinda Urusi. 

Hii ndio mara ya Kwanza, kwa Umoja wa Ulaya kufanya kikao chake jijini Kyiv, tangu Urusi ilipoivamia Ukraine karibu mwaka mmoja uliopita. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.