Pata taarifa kuu
URUSI- UKRAINE- MAPIGANO

Ukraine: Nchi washirika zimekubali kutoa ndege za kivita kulinda ardhi yetu

Waziri wa ulinzi wa Ukraine, Oleksii Reznikov, amesema nchi washirika zimekubali kutoa ndege za kivita kukabiliana na mashambulio ya Urusi, licha ya hivi karibu nchi za magharibi kudai hazina mpango wa kutoa ndege kwa utawala wa Kiev.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na mkuu wa tume ya umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na mkuu wa tume ya umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen AFP - SERGEI SUPINSKY
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Reznikov, ameitoa wakati huu Urusi ikijiandaa kwa mashambulio zaidi katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

“Nadhani tayari mmesoma yakwamba siku ya Ijuma washirka wetu wa Marekani walitupa silaha za masafa marefu zenye uwezo wa kufyatua risasi umbali wa kilomita 130.”ameeleza Oleksii Reznikov.

Katika hatua nyingine, wabunge wamempendekeza mkuu wa idara ya usalama, Kyrlo Budanov, kuwa waziri mpya wa ulinzi, baada ya waziri Reznikov kutuhumiwa kwa rushwa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.