Pata taarifa kuu

Ukraine: Mgahawa mmoja wakumbwa na shambulio baya Kramatorsk

Shambulio la anga la jeshi la Urusi dhidi ya mgahawa huko Kramatorsk, mashariki mwa Ukraine, ulisababisha vifo vya watu tisa na 56 kujeruhiwa siku ya Jumanne, kulingana na ripoti iliyotolewa Jumatano, Juni 28 na idara ya huduma za dharura.

Picha imetolewa na utawala wa jimbo la Donetsk la Ukraine, kwenye barabarani nje ya duka la Pizza na mkahawa wa RIA ulioharibiwa na shambulio la Urusi huko Kramatorsk, Ukraine, Jumanne, Juni 27, 2023.
Picha imetolewa na utawala wa jimbo la Donetsk la Ukraine, kwenye barabarani nje ya duka la Pizza na mkahawa wa RIA ulioharibiwa na shambulio la Urusi huko Kramatorsk, Ukraine, Jumanne, Juni 27, 2023. AP - Donetsk regional administration
Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya Kremlin imesema leo Jumatano ilitekeleza shambulio hilo dhidi kambi ya jeshi nchini Ukraine baada ya mgahawa mmoja kubomolewa kwa hambulio usiku wa kuamkia jana huko Kramatorsk mashariki, shambulio ambalo liligharimu maisha ya watu kumi na 61 kujeruhiwa. "Urusi hailengi miundombinu ya kiraia, inashambulia mitambo ambayo kwa namna fulani vinahusishwa na miundombinu ya kijeshi," msemaji wa rais wa Urusi Dmitry Peskov amewaambia waandishi wa habari.

Kulingana na polisi ya Ukraine, Urusi ilirusha makombora mawili ya S-300 huko Kramatorsk, mji ambao ulikuwa na wakazi 150,000 kabla ya vita kuingia mwezi wake wa kumi na sita.

Miongoni mwa waliouawa ni watoto watatu, idara ya huduma za Dharura nchini Ukraine imesema kwenye Telegram. "Waokoaji wanachimba vifusi vya jengo lililoharibiwa na kutafuta watu ambao huenda wamekwama chini ya vifusi," idara ya huduma za Dharura imeongeza. Shambulio hilo lliharibu mkahawa wa Ria Pizza, kituo kilicho katikati ya Kramatorsk maarufu kwa wanahabari na wanajeshi.

Maafisa watatu kutoka Colombia, mwandishi maarufu Hector Abad, mwanasiasa Sergio Jaramillo na mwanahabari Catalina Gomez, mwandishi wa habari nchini Ukraine wa RFI/F24 kwa lugha ya Kihispania na gazeti la kila siku la El Tiempo, walijeruhiwa kidogo walipokuwa wakila kwenye mgahawa huo na mwandishi wa Ukraine Victoria Amelina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.