Pata taarifa kuu

Yevgeny Prigozhin mkuu wa Wagner yuko uhamishoni nchini Belarus

Nairobi – Kiongozi wa mamluki wa Wagner, aliyekuwa amepanga kulipindua jeshi la Urusi wiki iliyopita, Yevgeny Prigozhin, hatimatiye amewasili nchini Belarus, huku jeshi la pamoja la nchi za Magharibi NATO likisema liko tayari kujilinda dhidi ya Moscow au Minsk.

Yevgeny Prigozhin, amewasili nchini Belarus
Yevgeny Prigozhin, amewasili nchini Belarus © ALEXANDER ERMOCHENKO / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kuwasili kwa Prigozhin nchini Belarus, kumekuja wakati huu Urusi ikipanga kulivunja kundi hilo la wapiganaji, ambalo rais Vladimir Putin kwa mara ya kwanza amekiri kuwa limekuwa likifadhiliwa na serikali.

Kiongozi wa Belarus Alexander Lukashenko, amethibitisha kuwasili kwa kiongozi wa kundi hilo na kuongeza kuwa alimsihi Putin asimuue, baada ya jaribio la wapiganaji wake kutoka kufika Moscow.

Rais wa Belarus amethibitisha kuwasili kwa mkuu wa mamluki wa Wagner nchini mwake
Rais wa Belarus amethibitisha kuwasili kwa mkuu wa mamluki wa Wagner nchini mwake via REUTERS - PRESIDENT OF BELARUS PRESS SERVI

Wakat hayo yakijiri, Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg, amesema Jumuiya hiyo itafuatilia kwa makini matukio yote yanayoendelea, na iwapo vikosi vya Wagner vitakwenda Belarus na kutishia washirika wake.

Katika hatua nyingine, wanajeshi wa Urusi wameendelea kurusha makombora yake nchini Ukraine, ambapo wamesababisha vifo vya watu wanne katika mji wa Kramatorsk.

Moscow inasema licha ya jaribo la kujaribu kuangusha jeshi na uongozi wake na kundi la Wagner, mipango yake itaendelea nchini Ukraine kama kawaida.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.