Pata taarifa kuu

Afrika: UN yaonya kutokea athari iwapo mkataba wa nafaka wa bahari nyeusi utasitishwa

Nairobi – Mataifa ya Pembe ya Afrika huenda yakakabiliwa na athari kubwa iwapo mpango wa usafirishaji wa nafaka kupitia bahari nyeusi utasitishwa.

Urusi imekuwa ikitishia kuachana na mpango huo
Urusi imekuwa ikitishia kuachana na mpango huo REUTERS - YORUK ISIK
Matangazo ya kibiashara

Maofisa katika ukanda huo wameonya kuwa hatua hiyo huenda ikasababisha kuongezeka kwa bei za bidhaa hali ambayo itakuwa tishio kwa maelfu ya raia wanaokabiliwa na uhaba wa chakula.

Moscow kwa muda sasa imekuwa ikitishia kuachana na mpango huo ambao ulianzishwa na Umoja wa Mataifa na Uturuki mwezi Julai mwaka jana iwapo vikwazo kuhusu usafirishaji wa nafaka yake na mbolea havitaondolewa.

Kwa upande wake, mjumbe wa Ukraine amesema kuwa kuna uwezekano wa asilimia 99.9 kwamba Urusi itaondoka katika makubaliano hayo ifikapo tarehe 18 ya mwezi Julai muda ambao yanapaswa kufanya upya.

Mataifa ya Pembe ya Afrika yanatarajiwa kuendelea kukabiliwa na baa la njaa baada ya msimu wa mvua uliotarajiwa mwezi Aprili kufeli.

Mashirika ya misaada yanasema kuwa karibia watu milioni sitini wanakabiliwa na uhaba wa chakula katika mataifa saba ya Afrika Mashariki na huenda hali ikawa mbaya Zaidi iwapo mpango huo wa usafirishaji wa nafaka katika bahari nyeusi utasitishwa.

Takwimu za Umoja wa mataifa zinaonyesha kuwa karibia tani laki saba za nafaka zimesafirishwa katika mataifa ya Kenya na Ethiopia tangu kuaanza kwa mkataba huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.