Pata taarifa kuu

Urusi: Putin atoa pendekezo kwa mamluki wa Wagner kujiunga na Jeshi au kwenda Belarus

Katika hotuba, Rais wa Urusi Vladimir Putin ametoa pendekezo kwa wapiganaji wa kundi la Wagner kujiunga na jeshi la Urusi au kumfuata kiongozi wao, Yevgeny Prigozhin, nchini Belarus.

Rais wa Urusi Vladimir Putin, wakati wa hotuba yake mnamo Juni 26, 2023.
Rais wa Urusi Vladimir Putin, wakati wa hotuba yake mnamo Juni 26, 2023. AFP - NATALIA KOLESNIKOVA
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba fupi ya televisheni, Vladimir Putin ameamua kuweka wazi msimamo wake kwa mamluki wa Wagner akiwaambia wachaguwe kwenda uhamishoni nchini Belarus wakiambatana na mkuu wao Yevgeny Prigozhin, huku akiwataka wajiunge na jeshi la Urusi.

Rais wa Urusi amesema Jumatatu kuwa amegiza "kuepusha damu" ni hali ambayo Ukraine na nchi za Magharibi walikuwa wakifurahia hali hiyo itokee wakati wa uasi wa kundi la Wagner. Amewashukuru Warusi kwa "uzalendo" wao na umoja wao. "Tangu kuanza kwa matukio, hatua zilichukuliwa kwa maagizo yangu ya moja kwa moja ili kuzuia damu kubwa zisimwagike," Valdimir Putin amesema.

Hakusema chochote juu ya hatima ya Yevgeny Prigozhin, wala waziri wake wa ulinzi, Sergei Choigou, au mkuu wa majeshi, Jenerali Valéry Guerassimov, ambao mkuu wa Wagner alikuwa akidai wauawe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.