Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Mapigano yaripotiwa katika jimbo la Voronezh nchini Urusi

Gavana wajimbo la Voronezh, lililoko takriban kilomita 600 kusini mwa Moscow, ametangaza siku ya Jumamosi kuwa vikosi vya Urusi vinapigana kama sehemu ya operesheni ya kupambana na ugaidi iliyoanzishwa baada ya kuingia katika uasi wa kundi la wanamgambo la Wagner. Hapo awali, kiongozi wake Yevgeny Prigozhin alisema amechukua udhibiti wa eneo la Rostov-on-Don.

Wapiganaji wa kundi la Wagner wakitumwa katika jiji la Rostov-on-Don mnamo Juni 24, 2023.
Wapiganaji wa kundi la Wagner wakitumwa katika jiji la Rostov-on-Don mnamo Juni 24, 2023. AFP - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Unachopaswa kufahamu:

• Katika mfululizo wa jumbe za sauti, kiongozi wa Kundi la Wagner Yevgeny Prigozhin ametoa wito wa uasi dhidi ya uongozi wa jeshi la Urusi. Anashutumu jeshi kwa kushambulia kambi za kijeshi za kundi la Wagner. Akidai kuongoza "maandamano ya kutafuta haki" na sio "mapinduzi ya kijeshi", Yevgeny Prigozhin anasema "yuko tayari kufa" na wapiganaji wake 25,000 kwa minajili ya "kuwakomboa raia wa Urusi".

• Gavana wa jimbo la Voronezh ameripoti mapigano ya wanajeshi wa Urusi. Mapema asubuhi, kiongozi wa Wagner alitangaza kwamba vikosi vyake vilivyowekwa nchini Ukraine hadi sasa vimevuka mpaka na kuingia Rostov, yalipo makao makuu ya kamandi ya kusini ya jeshi la Urusi, ambapo shughuli za kijeshi nchini Ukraine zinaratibiwa.

• Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Urusi imetangaza kufunguliwa kwa uchunguzi kuhusu "uasi wa kutumia silaha" dhidi ya Yevgeny Prigozhin.

• Katika hotuba kwa taifa, Rais Vladimir Putin ameahidi hataruhusu "vita vya wenyewe kwa wenyewe" kutokea na kutoa wito wa "umoja". Akiuita uasi wa Wagner kuwa "tishio kuu", amemshutumu Yevgeny Prigozhin kwa "kusaliti" Urusi kwa sababu ya "matamanio yake mengi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.