Pata taarifa kuu

Vikwazo: Moscow yapanua orodha yake ya maafisa wa Ulaya waliopigwa marufuku kuingia Urusi

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ursi imetangaza kuwa imepanua orodha ya watu waliopigwa marufuku kuingia katika ardhi yake ili kukabiliana na awamu ya kumi na moja ya vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Moscow, na kuongeza kuwa itachukua hatua mpya za kulipiza kisasi kwa wakati ufaao.

Rais wa Urusi Vladimir Putin ahudhuria mkutano na wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu vya kijeshi vya nchi hiyo katika Kremlin mjini Moscow, Urusi Juni 21, 2023.
Rais wa Urusi Vladimir Putin ahudhuria mkutano na wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu vya kijeshi vya nchi hiyo katika Kremlin mjini Moscow, Urusi Juni 21, 2023. via REUTERS - SPUTNIK
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake, wizara hiyo imesema orodha hiyo ni pamoja na maafisa wa usalama, watumishi wa umma, wafanyabiashara na wabunge wa Bunge la Ulaya.

Wakati huo huo Ukraine inadai kuangusha zaidi ya makombora kumi na mbili ya cruise ya Urusi usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa. Makombora haya yalilenga uwanja mdogo wa ndege wa kijeshi magharibi mwa nchi, kulingana na Jeshi la Wanahewa.

Kwingineko jeshi la Urusi linarudi nyuma katika maeneo kadhaa ya kusini na mashariki mwa Ukraine, anasema kiongozi wa kundi la wanamgambo la Wagner, akipingana na matamshi ya Kremlin kwamba mashambulio ya Kiev yalishindwa.

"Jeshi la [Urusi] linajiondoa katika maeneo ya Zaporizhia na Kherson, wanajeshi wa Ukraine wanasonga mbele," Yevgeny Prigozhin amesema katika mahojiano ya video yaliyotumwa kwenye Telegram na hidara yake ya vyombo vya habari.

"Hali kama hiyo inafanyika huko Bakhmout, adui atapenya zaidi na zaidi katika ulinzi wetu," mfanyabiashara huyo ameongeza, akimaanisha mji wa mashariki ambao Warusi wanadai kuwa wameuteka lakini Waukraine wanasema wamepiga hatua kwenye ukingo katika wiki za hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.