Pata taarifa kuu

Msaada mkubwa wa ujenzi mpya kwa Ukraine wawasili katika mkutano wa London

Mataifa sitini, makampuni 400, wajumbe elfu moja wanakusanyika Jumatano hii Juni 21 na Alhamisi Juni 22 katika mji mkuu wa Uingereza, London, kwa ajili ya mkutano juu ya ujenzi wa Ukraine. Lengo ni kuwahakikishia wawekezaji na kujiandaa kwa ajili ya kuimarika kwa uchumi wa nchi hii pindi vita vitakapomalizika. Rais wa Ukraine amezindua siku hizi mbili za majadiliano.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ahudhuria hotuba ya Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak kwa njia ya video kwenye Kongamano la Urejeshaji wa Ukraine mjini London, Jumatano, Juni 21, 2023.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ahudhuria hotuba ya Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak kwa njia ya video kwenye Kongamano la Urejeshaji wa Ukraine mjini London, Jumatano, Juni 21, 2023. AP - Leah Millis
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ambaye ameonekana kwenye video, amewahutubia wadau wa "kisiasa, kiuchumi na viongozi mbalimbali" waliokusanyika London, anaripoti mwandishi wetu huko London, Émeline Vin. "Kwa kuijenga upya Ukraine, tutajenga upya uhuru. Rais wa Ukraine anatarajia, pamoja na mkutano huu, kushawishi makampuni na wawekezaji kurejea nchini. "Utulivu wa kimataifa unategemea utulivu wa Ukraine," amekumbsha, akimaanisha kwa mfano kilimo na uzalishaji wa nishati.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Rais wa Tume ya Ulaya, wakuu wa diplomasia wa Marekani, Ufaransa, Poland na Japan, wote walifuatana jukwaani kukumbusha mshikamano wao na Ukraine. Ingawa sio mkutano rasmi wa wafadhili, nchi kadhaa zimejikubalisha kukamilisha ahadi zao: Ufaransa imewasilisha utaratibu wa bima unaoungwa mkono na Benki ya Maendeleo ya Ufaransa

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak ametangaza dhamana ya mkopo wa benki ya euro bilioni 3 kwa Ukraine. Ujenzi mpya unakadiriwa kuwa bilioni 400 kwa miaka kumi.

Kyiv itabidi ihakikishe

Kwa upande wake, Marekani itatoa msaada wa dola bilioni 1.3 (euro bilioni 1.2) kama msaada wa ziada kusaidia uchumi wa Ukraine, hususan miundombinu yake muhimu, Waziri wa Mambo ya Nje amesema Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken siku ya Jumatano wakati wa mkutano huo. "Maadamu Urusi inaendelea kuharibu, tutakuwepo kusaidia Ukraine kuijenga upya: kujenga upya maisha, kujenga upya nchi yao, kujenga upya maisha yao ya baadaye," Antony Blinken amesema.

Mataifa yanadai kutaka kufufua uchumi wa Ukraine, hasa kukarabati mtandao wake wa umeme na nishati ambao umeharibiwa kwa kiasi kikubwa na milipuko ya mabomu. Makubaliano pia yanaibuka: wazo la kuifanya Urusi kulipa kwa ujenzi mpya. Hata hivyo, London inatarajiwa kutangaza vikwazo vipya vinavyolenga viongozi wa Urusi mapema wiki ijayo.

Siku iliyosalia huchukua mfumo wa vikao vya mashauriano: uwazi na mageuzi, mfumo wa ufufuaji endelevu, fursa za uwekezaji na mbinu za kupambana na hatari kwa sekta binafsi. Matoleo mapya ya kitaifa yanapaswa kuwasilishwa mwishoni mwa siku.

Mbali na operesheni ya upotoshaji kwa makampuni, Ukraine italazimika kuwahakikishia washirika wake wa kimataifa kuhusu afya ya taasisi zake.

Mkutano huu wa ujenzi mpya, ambao tayari ulikuwa umefanyika mwaka jana huko Lugano, Uswisi, ndio mrithi wa Mkutano wa Marekebisho, wa kutokomeza ufisadi: mnamo 2021, kabla ya vita, shirika lisilo la kiserikali la Transparency International liliiweka Kiev katika kiwango sawa na Mexico au Ufilipino.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.